Mkutano wa Mawaziri wa
Kamati ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ya Asasi ya Ushirikiano
wa Siasa, Ulinzi na Usalama kwa ngazi ya Mawaziri umefanyika kwa njia ya
Mtandao (Video Conferencing) na kujadili masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama.
Mkutano huo umefanyika chini
ya Uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa wa Jamhuri ya
Zimbabwe, Mhe. Sibusiso Busi Moyo na utakutanisha Mawaziri wenye dhamana ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mambo ya Ndani, Ulinzi pamoja na
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoka nchi wanachama wa SADC. Ujumbe wa
Tanzania umeongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi.
Mkutano huo umehudhuriwa
na nchi 16 wanachama wa SADC ambazo ni Angola, Afrika Kusini, Botswana, Comoro,
DRC, Eswatini, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Madagascar, Namibia,
Visiwa vya Shelisheli, Zambia, Zimbabwe na Mwenyekiti Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Mawaziri pamoja
na baadhi ya Makatibu Wakuu/Maafisa waandamizi kutoka Tanzania wakifuatilia
mkutano kwa njia ya Video Conference, jijini Dar es Salaam
|
Mkutano
ukiendelea
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.