Tanzania imejivunia mafanikio yaliyopatikana wakati ikiwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Mafanikio
hayo yameelezewa katika Mkutano wa 40 wa Baraza la Mawaziri na Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi ulifanyika
kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam.
Kupitia
mkutano huo, Prof. Kabudi amekabidhi
uenyekiti wa Baraza la Mawaziri kwa Balozi wa Msumbiji nchini, Mhe. Monica P.
Clemente kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji Mhe. Verónica Nataniel
Macamo Dlhovo
Prof.
Kabudi amesema pamoja na janga la ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID 19)
jumuiya ya SADC imeendelea kufanya kazi zake, mikutano yake chini ya uongozi wa
Tanzania kwa ufanisi wa hali ya juu kwa kupitia njia ya mtandao (video
conference)
"Nasema
ni mafanikio makubwa kwa sababu Jumuiya nyingine za kikanda zimeshindwa kufanya
hivyo, sisi ndiyo jumuiya pekee iliyoanza utaratibu huu wa aina hii ya mikutano
kwa sababu kwetu tuliona COVID 19 ni changamoto ambayo haiwezi kutuzuia kufanya
shughuli zetu,". Amesema Prof. Kabudi
Prof.
Kabudi ameongeza kuwa mbali na kupambana a janga la COVID 19, mafanikio mengine
ni kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya nne katika jumuiya ya SADC,
lugha nyingine ni Kiingereza, Kireno na Kifaransa.
"Lugha
ya Kiswahili kwa Tanzania ni lugha ya ukombozi wa Afrika, ndiyo lugha
iliyotumika wakati wa kuwafundisha wapigania uhuru mbinu za kuwasiliana wakati
wa ukombozi kwa mataifa ya Afrika," Amesema Prof. Kabudi.
Prof.
Kabudi ameyataja mafanikio mengine yaliyopatikana wakati Tanzania ikiwa
mwenyekiti wa SADC ni kusimamia na kukamilika kwa Mwongozo wa kusafirisha
bidhaa na huduma kwa nchi wanachama katika kipindi cha (COVID-19). Mwongozo huo
umelenga kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona na kurahisisha
usafirishaji wa bidhaa na huduma mbambali baina ya nchi wanachama.
Tanzania
imewezesha agenda ya viwanda kutekelezwa ambapo wakati wa COVID 19 tumeweza
kuongeza uwezo wetu wa kutengeneza dawa kwa kuwa mataifa makubwa duniani mara
baada ya kuibuka kwa covid 19 walisitisha kuuza dawa katika nchi nyingine ili
wazitumie dawa hizo ndani ya nchi zao.
"Tunaimani
kuwa msingi uliowekwa wakati wa COVID 19 utaimarisha jitiada zetu za kuwa na uchumi
wa viwanda, uchumi wa kati na uchumi wa juu. Na sisi imekuwa jambo la faraja
kubwa kuingia katika uchumi wa kati kabla ya miaka mitano iliyokuwa imepangwa
hapo awali," Amesema Prof. Kabudi.
"Chaguzi
katika nchi za Malawi, Mauritius, Namibia zimefanyika kwa amani na utulivu. Ii
imedhihirisha wazi kuwa demokrasia katika ukanda wetu inazidi kukua………haya yote
ni mafanikio makubwa kwetu tukiwa mwenyekiti wa SADC," ameongeza Prof.
Kabudi.
Nae
Balozi wa Msumbiji nchini, Mhe. Monica Clemente aliyemuwakilisha Waziri wa
Mambo ya Nje Msumbiji, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi kubwa aliyofanya wakati wa
Uenyekiti wake wa SADC.
Amefanya
mambo makubwa kabisa kwa nchi wanachama wa SADC na amekuwa kama Mwalimu kwa
nchi nyingine kutokana na maendeleo yaliyopatikana wakati wa uongozi wake akiwa
mwenyekiti wa SADC.
"Sisi
Msumbiji tunashukuru kwa kupokea Uenyekiti wa SADC na tunaahidi kujitahidi
kadri ya uwezo wetu kuendeleza yale yote yaliyofanywa na Tanzania wakati akiwa
Mwenyekiti, kwani Tanzania amekuwa mwalimu kwetu na nchi nyingine za SADC,"
amesema Balozi Monica.
Mkutano wa 40 wa baraza la mawaziri umehudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Waziri wa Afya , Maendeleoya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa wakifuatilia mkutano kwa njia ya Mtandao (Video Comnference)
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi akifungua mkutano wa 40 wa Baraza la Mawaziri uliofanyika jijini Dar
es Salaam kwa njia Mtandao (Video Comnference)
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akikabidhi uenyekiti wa SADC ngazi ya mawaziri kwa Balozi wa Msumbiji nchini, Mhe. Monica P. Clemente ambaye amemwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje Msumbiji Mhe.Verónica Nataniel Macamo Dlhovo
Baadhi ya viongozi waandamizi wa Serikali wakifuatilia Mkutano wa 40 wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa wakifuatilia mkutano kwa njia ya Mtandao (Video Conference)
Baadhi ya maafisa waandamizi/Makatibu Wakuu wakifuatilia mkutano wa 40 wa Baraza la Mawaziri uliofanyika leo kwa nnjia mtandao jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.