Dkt. Haji ameongoza ujumbe wa Tanzania kwenye kikoa cha Kanda cha Makatibu Wakuu wa Jamuiya ya Afrika Mashariki kujadili namna bora ya kuendelea na majadiliano ya biashara baina ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Uingereza.
Lengo la majadiliano baina ya Afrika Mashariki na Uingereza ni kuwa na Mkataba wa Biashara utakaowezesha Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuuza bidhaa kwenye Soko la Uingereza na Uingereza kwenye Soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki kuanzia tarehe 01 Januari, 2021.
Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa muda mrefu imekuwa mshirika mzuri wa biashara kwa nchi ya Uingereza. Hata biashara hiyo biashara hiyo awali imekuwa ikifanyika kwa kufuata sheria, miongozo na taratibu za Umoja wa Ulaya. Kufauatia hatua ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya imeenda sera na mwongozo mpya utakao ifanya nchi hiyo kuendelea kufanya biashara na Mataifa mbalimbali.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.