Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeihakikishia Uingereza pamoja na Jumuiya ya Kimataifa kuwa uchaguzi mkuu unaotegemewa kufanyika mwezi Oktoba mwaka 2020 utafanyika kwa amani, uhuru na haki.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi wakati akipokea
nakala za hati za utambulisho za Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Mhe.
David Concar
Prof
Kabudi amesema kuwa paamoja na mambo mengine, amemhakikishia balozi mteule wa
Uingereza nchini Mhe. Concar kuwa mchakato wa uchaguzi nchini unaendelea vizuri
sana ambapo mikutano ya kampeni imeanza kwa ngazi zote (ngazi ya uchaguzi wa
Rais, Wabunge na Madiwani) na mpaka sasa kampeni zinaendea vizuri.
"kama
ilivyoada ya watanzania nimemhakikishia kuwa uchaguzi huu utafanyika kwa amani
na utulivu na mwisho wa siku maamuzi yatakayotolewa na watanzania ya kuamua
nani awe diwani, nani awe mbunge na nani awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
yataheshimiwa na watanzania wote," Amesema Prof. Kabudi.
Kwa
upande wake Balozi mteule Mhe.David Concar amesema kuwa katika maongezi yao
mbali na kugusia suala la uchaguzi pia wameongelea namna ya kuimarisha
mahusiano baina ya Tanzania na Uingereza na mazingira bora ya kuvutia zaidi
wawekezaji kuja nchini,kukuza biashara hususani baada ya Uingereza kujitoa
katika jumuiya ya Umoja wa Ulaya na pia kusaidia maendeleo katika maeneo ya
afya,maji pamoja na elimu.
Katika
hatua nyingine Prof. Kabudi amepokea nakala za hati za utambulisho za Balozi
Mteule wa Pakistan hapa Nchini Mhe. Mohamed Saleem.
Katika
mazungumzo hayo Prof. Kabudi amesema kutokana na Pakistan kupiga hatua kubwa ya
kimaendeleo katika viwanda vya mbolea wamekubaliana kuangalia namna ya
kushirikiana ili kujenga viwanda vingi vya mbolea hapa nchini pamoja na kufanya
biashara ya moja kwa moja ya zao la chai badala ya kupitia katika masoko ya minada
ya Afrika Mashariki.
Kwa
upande wake Balozi wa Pakistan nchini, Mhe. Mohhamed Salim amesema atahakikisha
kuwa Tanzania na Pakistan zinaendelea kuimarisha diplomasia ya uchumi kwa
kuwawezesha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi zote mbili ili kuweza
kunufaika na furza za kukuza uchumi.
Hafla
ya mabalozi wateule kukabidhi hati za utambulisho pia ilihudhuriwa na Katibu
Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Brigedia Jenerali, Wilbert Ibuge.
Balozi mteule wa Uingereza nchini Mhe. David Concar akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi leo jijini Dar es Salaam
Balozi mteule wa Uingereza nchini Mhe. David Concar akimkabidhi nakala ya hati za utambulisho Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali, Wilbert Ibuge (kulia) akifuatilia maongeza mara baada ya Mabalozi wateue kuwasilisha hati za utambulisho kwa Waziri Prof. Kabudi
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.