Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Balozi
Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge wamesaini kitabu cha maombolezo Ubalozi wa India
nchini kufuatia kifo cha Rais mstaafu wa Taifa hilo Shri Pranab Mukherjee kilichotokea
tarehe 31 Agosti 2020.
Akizungumza mara baada ya kusaini kitabu cha
maombolezo katika ubalozi ubalozi wa India nchini, Jijini Dar es
Salaam Prof. Kabudi ametoa pole kwa wananchi wote wa India na kuwasihi
kuendelea kuwa watulivu na wastahimilivu wakati huu wa msiba wa kiongozi wao
mstaafu.
"Kusaini kitabu cha maombolezo ni ishara ya
ushirikiano wetu, umoja wetu na undugu wetu na ndugu zetu wa India. Kifo cha
Rais Shri Pranab Mukherjee kinawahusu pia watanzania kwa sababu Tanzania na
India zina uhusiano mzuri, imara na wa muda mrefu ulianzishwa na baba wa Taifa
Mwl. Julias Nyerere pamoja na Mahatma Gandhi,” amesema Prof. Kabudi
Rais Shri Pranab Mukherjee ni miongoni mwa viongozi
wa zamani wa India waliowahi kufanya kazi katika Serikali ya Waziri Mkuu wa
Zamani Indira Gandhi aliyewahi kukabidhiwa nyadhifa mbali mbali ikiwemo Waziri
katika Sekta tofauti.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akisaini kitabu cha maombolezo katika
ubalozi wa India nchini Tanzani. Pembeni yake kulia ni Balozi wa India nchini
Mhe. Shri
Sanjiv Kohli
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akisaini kitabu cha
maombolezo katika ubalozi wa India nchini Tanzania
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.