Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeahidi kuendelea kuisaidia Congo kulinda amani na kuhakikisha changamoto za ulinzi na usalama zinazoikabili nchi hiyo zinatatuliwa ili kuimarisha hali ya amani katika Ukanda wa Maziwa Makuu.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) alipokuwa akimwakilisha Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika Mkutano
wa Nane wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa
Maziwa Makuu (ICGLR) uliofanyika kwa njia ya video (Video Conference).
"Tanzania
tutaendelea kusaidia juhudi za kuimarisha ulinzi na usalama katika eneo la
mashariki mwa Congo - DRC kwani kukosekana kwa utulivu wa kisiasa na kiusalama
kwa nchi hiyo kunahatarisha usalama wa eneo lote la Jumuiya nzima ya ICGLR nayo
itakuwa salama," amesema Prof. Kabudi.
Ameongeza
kuwa Congo Brazaville ilikuwa ikikabiliwa na uasi kutoka kundi la Ninja
lililokuwa likiisumbua Serikali kwa miaka mingi hata hivyo hadi kufikia
katikati ya mwaka 2019 uasi ulitulia kufuatia mazungumzo ya kusitisha mapigano kati ya kundi hilo na Serikali.
Amesema
Congo-Kinshasa na Congo-Brazaville ni muhimu katika eneo la maziwa makuu
kutokana na kuwepo kwa asilimia kubwa ya rasilimali za misitu, maji na madini
ambavyo vinahitajika sana duniani na kuongeza kuwa umuhimu zaidi unahitajika
kutokana na ukweli kuwa kuna haja kubwa ya kutunza mazingira, kuzalisha nishati
na kukuza uchumi wa dunia.
"Nchi
hizi mbili za DRC na Congo Brazaville ni nchi muhimu sana katika eneo la Maziwa
Makuu kutokana na kuwepo kwa asilimia kubwa ya rasilimali, baadhi ya rasilimali
hizo kama misitu, maji na madini zinahitajika sana duniani kwa sasa kutokana na
umuhimu wake, umuhimu ambao unatokana na haja ya kutunza na kulinda mazingira, uzalishaji wa nishati na
kukuza uchumi wa dunia," alisema n kuongeza kuwa Kukosekana kwa utulivu wa
kisiasa na kiusalama katika nchi hizi kunahatarisha usalama wa eneo lote la Maziwa
Makuu ikiwemo na usalama wa dunia kutokana na uwezekano wa baadhi ya mataifa
makubwa kugombea rasilimali hizo", alisisitiza Prof. Kabudi.
Mkutano
huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya ICGLR umepokea na kujadili taarifa
mbalimbali kuhusu Jumuiya hiyo , mbali na hali ya kisiasa na kiusalama katika Ukanda
huo umeangalia pia suala la michango ya wanachama katika bajeti ya Sekretariat
na Mfuko Maalum wa maendeleo, taarifa ya mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa
Jumuiya, taarifa ya mkutano wa Mawaziri wa Ulinzi kuhusu hali ya usalama wa Ukanda wa Maziwa
Makuu na taarifa ya mkutano wa Mawaziri wa Afya.
Nchi
wanachama wa ukanda wa maziwa makuu ni pamoja na Angola, Burundi, Jamhuri ya
Kati, Demokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kongo, Kenya, Rwanda, Sudan, Sudani
Kusini, Tanzania, Uganda na Zambia.
Oktoba
2019, Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu
ulifanyika nchini Congo Brazzaville.
Katika
tukio jingine, Prof. Kabudi amekutana na kumuaga Mwakilishi Mkazi wa Benki ya
Maendeleo Afrika (AfDB), Bw. Alex Mubiru ambapo pamoja na mambo mengine
amemshukuru Bw. Mubiru kwa mema aliyoyafanya hapa nchini hasa katika
kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua kimaendeleo.
Rais
wa Jamhuri wa Kidemokrasia ya Kongo, Mhe. Felix Tshisekedi akizungumza katika
mkutano wa Nane wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda
wa Maziwa Makuu (ICGLR)
Katibu
Mkuu Umoja wa Mataifa Bw. António Guterres akizungumza katika mkutano wa Nane wa
Kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu
(ICGLR) |
Rais
wa Jamhuri wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame akizungumza katika mkutano wa Nane wa Kawaida
wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.