Tanzania na Indonesia zimeahidi kushirikiana na kuendeleza kukuza biashara kwa kuanzisha kwa manufaa ya nchi zote mbili.
Akihutubia
katika usiku wa shukrani kwa ajili ya wafanyabiashara wa Tanzania na Indonesia
kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kukuza biashara na uwekezaji kati ya nchi
hizo mbili, Balozi
wa Indonesia nchini Tanzania Mhe. Prof. Ratlan Pardede amesema kuwa maendeleo
yaliyopatika kwenye sekta ya biashara nzuri inayofanywa na wafanyabiashara
kutoka nchi zote mbili.
"Sisi
Indonesia na Tanzania tumekuwa tukifanya biashara yenye manufaa kwa mataifa
yetu mawili, bidhaa tunazouza ni imara na zimekuwa na ubora mzuri ambapo kwa
sasa biashara imeongeza mapato zaidi ya asilimia 10," Amesema Balozi Pardede
Ameongeza
kuwa mwaka 2017 aliahidi kuwaleta wafanyabiashara na wawekezaji kutoka
Indonesia kuja Tanzania kwa ajili ya kuwekeza, ambapo hadi sasa tayari wameanzisha
kiwanda cha Sabuni na Losheni Mkuranga
Kwa
upande wake Mgeni Rasmi, ambaye ni Waziri wa Biashara na Uwekezaji kutoka
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga amempongeza
Balozi kwa hatua na mipango mizuri ya kuinua uchumi wa mataifa yote mawili na
kumuahidi ushirikiano katika kuhakikisha kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea
kuwaboreshea mazingira wawekezaji na wafanyabiashara ili kuwawezesha kufanya
biashara vizuri katika mazingira salama.
Nataka
nikuhakikishie kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara kati ya
Indonesia na Tanzania kwa kiwango cha juu." Amesema Soraga. Pia Mhe.
Waziri alielekeza wakati mwingine Baraza la kuundwe Biashara la Tanzania na
Indonesia (TIBC) ili mpango huo uweze kujumuisha zaidi na kuwafikia wadau wengi
nchini Tanzania.
Kulingana
na rekodi za Ubalozi wa Indonesia, bidhaa takribani 54 za Kiindonesia zipo
kwenye soko la Tanzania kama vile mafuta ya Mawese, nguo, karatasi pamoja na
sabuni. Kwa upande mwingine, Indonesia imekuwa ikiagiza bidhaa kadhaa kutoka
Tanzania, ambazo ni karanga, pamba, kakao, kahawa, chai, viungo na tumbaku.
Balozi
wa Indonesia nchini Tanzania Mhe. Prof. Ratlan Pardede akiongea na
wafanyabiashara (hawapo pichani) katika hafla ya usiku wa shukrani kwa ajili ya
wafanyabiashara wa Tanzania na Indonesia iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Biashara na Uwekezaji kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Mudrik
Ramadhan Soraga akihutubia hadhara ya wafanyabiashara (hawapo pichani) katika hafla
ya usiku wa shukrani kwa ajili ya wafanyabiashara wa Tanzania na Indonesia
iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Biashara na Uwekezaji kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Soraga akipokea
zawadi kutoka kwa Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mhe. Pardede jijini Dar
es Salaam
Waziri
wa Biashara na Uwekezaji kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Soraga (katikati)
akiwa pamoja na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mhe. Pardede katika picha
ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bw. Caesar Waitara
(kushoto) na Afisa Mkuu Mambo ya Nje, Bw. Francis Luangisa jijini Dar es Salaam
Washiriki
(wafanyabiashara) wakifuatilia mkutano
Baadhi ya Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Waziri Bw. Soraga pamoja na Mhe. Balozi, Pardede
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.