Ubalozi wa Tanzania, Qatar Washiriki Tamasha la Kumi la Kiasili la Majahazi
Ubalozi wa Tanzania Qatar ukishirikiana na Wanadiaspora
kutoka Tanzania unashiriki kwenye Tamasha la Kumi la Kiasili la Majahazi
lijulikanalo kama 10th Katara Traditional Dhow Festival.Tamasha hilo linafanyika Doha
kuanzia tarehe 1-5 Disemba 2020 ambapo Tanzania inaelezea utamaduni wa kiasili
wa jahazi wa mwambao wa Afrika Mashariki na Zanzibar ambapo ndio kitovu cha
utamaduni huo.
Utamaduni huo ulipelekea kuibuka muingiliano wa utamaduni wa lugha, mavazi, chakula na dini pamoja na matumizi ya Majahazi. Ubalozi umepata fursa pia ya kutangaza bidhaa za kitanzania kama viungo(spices) asali, korosho na kahawa pamoja na kutangaza utalii wetu.
Mgeni Rasmi, Mhe. Hamad bin Abdulaziz Al Kawari, Waziri wa Nchi
na Mkurugenzi wa Maktaba ya Taifa pamoja na Meneja Mkuu wa kijiji hicho cha
Katara, Dr. Khalid bin Ibrahim Al Sulaiti wakipata maelezo kwenye banda la Tanzania walipotembelea wakati wa uzinduzi wa Tamasha hilo.
Mabalozi wa Nchi za Afrika Mashariki waliopo Qatar wakiwa
katika picha ya pamoja kwenye Banda la Maonesho la Tanzania
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.