Na Mwandishi wetu,
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi
mbalimbali duniani kuongeza jitihada za kuhakikisha Diplomasia ya Uchumi
inaleta tija iliyokusudiwa.
Balozi
Ibuge ametoa kauli hiyo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo kwa nyakati
tofauti na Balozi wa Tanzania nchini Zimbambwe, Mhe. Prof. Emmanuel Mbennah
pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi katika Ofisi
ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Balozi
Ibuge katika mazungumzo yake na Balozi wa Tanzania nchini Zimbambwe Prof.
Mbennah amemtaka kuhakikisha kuwa anafanya kazi kwa weledi katika kuimarisha
uhusiano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Zimbabwe pamoja na
kukuza diplomasia ya uchumi kwa kuzingatia maelekezo ya Serikali.
“Balozi
nakusihi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kufanikisha azma na
malengo ya Serikali katika kuhakikisha tunaimarisha uhusiano wetu wa
kidiplomasia na Zimbabwe lakini pia kukuza diplomasia ya Uchumi kati yetu na
Zimbabwe,” Amesema Balozi Ibuge.
Kwa
upande wake, Balozi Prof. Mbennah amemhakikishia Katibu Mkuu kuwa uhusiano wa
Jamhuri ya Muungano na Tanzania na Zimbabwe ni mzuri na imara.
Katika tukio jingine, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili umuhimu wa kuhakikisha kuwa Tanzania inanufaika ipasavyo na uhusiano mzuri wa kidiplomasia ilionao na Marekani.
Katika kuhakikisha hilo, Balozi Ibuge alimsisitiza Balozi Masilingi kuendelea kufanya
kazi kwa bidii katika kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa manufaa ya Taifa.
Nae balozi Masilingi amemhakikishia Katibu Mkuu kuwa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani unaendelea kutekeleza diplomasia ya uchumi kwa kasi inayotakiwa.
Balozi
wa Tanzania nchini Zimbambwe Mhe. Prof. Emmanuel Mbennah akimuelezea jambo Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge wakati wa mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za
Wizara jijini Dar es Salaam
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge akiongea na Balozi wa Tanzania nchini Zimbambwe Mhe.
Prof. Emmanuel Mbennah
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini
Zimbambwe Mhe. Prof. Emmanuel Mbennah
Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akimuelezea jambo Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge wakati wa mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za
Wizara jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam. Kulia ni Msaidizi wa Katibu Mkuu Bi. Eva Ng’itu
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge akiongea na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe.
Wilson Masilingi
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini
Marekani Mhe. Wilson Masilingi
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.