Na Mwandishi wetu,
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge ameonesha kutoridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa
majengo ya mihadhara katika chuo cha Diplomasia na kumuagiza Mkandarasi anayetekeleza
mradi huo kuzingatia thamani ya fedha, muda wa mkataba na ubora.
Balozi
Ibuge ametoa maagizo kwa Mkandarasi huyo ambaye ni Kampuni ya Casco
Construction pamoja na mshauri muelekezi Ask architects wakati alipotembelea
mradi huo katika chuo cha Diplomasia leo jijini Dar es Salaam kusema kuwa endapo
Mkandarasi hata fanya hivyo atakuwa amekiuka masharti ya mkataba na mkataba
wake utasitishwa mara moja.
“Huu
mradi ni mradi wenye maslahi ya Taifa majadiliano yaishe leo mkataba ulishaisha
tangu mwezi Disemba 2020, hizi ni hela za walipa kodi…..nataka nione thamani
halisi ya fedha [Value for Money] ya walipa kodi katika mradi huu, siatakubali
kupoteza fedha za walipa kodi,” Amesema Balozi Ibuge
Katibu
Mkuu ameuagizo pia uongozi wa chuo hicho kuhakikisha kuwa unasimamia ujenzi wa
majengo hayo kwa karibu zaidi na umakini ili kuiwezesha serikali kupata thamani
halisi ya fedha katika mradi huo wenye maslahi mapana ya Taifa.
Awalia
akiongea na wahadhiri pamoja na wafanyakazi katika chuo hicho Balozi Ibuge
amewataka wote kwa pamoja kuhakikisha kuwa wanatekeleza diplomasia ya uchumi
kutokana na mabadiliko ya dunia.
“Najua
mmeanzisha mitaala inayogusia masuala ya diplomasia ya uchumi hadi mmeanza kuanzia
baadhi ya matawi katika baadhi ya mikoa hili ni jambo jema, lakini uwezo wa
nyinyi kuleta [link] ya utekelezaji wa diplomasia ya uchumi ambao ndiyo Wizara
yetu inasimamia…unapohusisha na nchi nyingine ni lazima utafiti wenu pamoja na
kuboresha wigo wa utekelezaji wa diplomasia ya uchumi,”
Balozi
Ibuge ameongeza kuwa diplomasia ya uchumia inaambatana na siasa pamoja na
diplomasia ya utamaduni wetu hasa kwenye lugha ya kiswahili hiyo ndiyo sehemu
ya mahusiano yetu na wengine.
“Urathi
wa ukombozi kusini mwa Afrika anayehusika ni Tanzania sasa Chuo cha Diplomasia
ambapo ndipo mawazo mazuri ya namna bora ya sisi kuhakikisha tunaiendeleza na
kuishindania na kuhakikisha hakuna mwingine wa kushindana na sisi, njia pekee
ni kupitia kwenu nyinyi na tafiti zenu,” Amesema Balozi Ibuge
Kwa
upande wake Mkandarasi anayetekeleza mradi huo Mhandisi Cosmas Salufu kutoka
kamupuni ya ujenzi ya Casco, pamoja na mshauri elekezi mhandisi Ally Simbano
kutoka kampuni Ask Architects kwa pamoja wameahidi kutekeleza maagizo ya Katibu
Mkuu na kuhakikisha kuwa thanami halisi ya fedha inapatikana katika mradi huo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge (aliyesimama) akiongea na wahadhiri pamoja na
wafanyakazi wa chuo cha Diplomasia leo Jijini Dar es Salaam wakati alipofanya
ziara chuoni hapo
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge akiongea na uongozi wa chuo cha Diplomasia leo Jijini
Dar es Salaam
Afisa
Miliki wa Chuo cha Diplomasia, Mhandisi Athumani Mashaka akimueleza jambo Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge wakati akitembelea mradi wa ujenzi wa majengo chuoni
hapo
Mhandisi
Cosmas Salufu pamoja na Mshauri Elekezi Mhandisi Ally wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge
wakati wa ziara ya ukaguzi wa majengo
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.