Na Mwandishi wetu,
Urari
wa kibiashara kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Saudia Arabia umezidi
kukuwa ambapo mpaka sasa miradi 14 ya uwekezaji kutoka nchini humo imesajiliwa
katika kituo cha taifa cha uwekezaji (TIC)huku kampuni nane za Kitanzania
zikipata kibali cha kuuza minofu ya samaki nchini humo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge ameyasema hayo katika mazungumzo yake na Balozi wa Saudi Arabia hapa nchini, Mhe.
Mohamed Bin Mansour Al Maliki anayemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini.
“Kwa
hakika kipindi hiki mahusiano ya Saudi Arabia na Tanzania yameimarika vizuri
kwa manufaa ya pande zote mbili, ambapo katika sekta ya uwekezaji kumekuwa na
miradi 14 iliyoandikishwa katika Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC) ambapo
uwiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Saudi Arabia unazidi
kuongezeka na kuimarika,” Amesema Balozi Ibuge
Balozi
Ibuge ameongeza kuwa zipo fursa nyingi za uwekezaji ambazo kupitia juhudi za
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na wadau wa
sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya kilimo, kampuni kubwa kampuni kubwa ya
Serikali ya Saudi Arabia ipo katika hatua za mwisho za kuja kuwekeza katika
sekta za mifugo na kilimo hapa nchini.
Balozi
Ibuge ameeleza kuwa kwa upande wa Tanzania “kampuni nane zimepata kibali cha
kuuza minofu ya samaki katika soko la Saudi Arabia ikiwa ni moja kati ya juhudi
ambazo zimekuwa zikifanywa na Balozi Al Maliki kwa kushirikiana na Serikali
katika kuimarisha mahusiano ya nchi zote mbili,”.
Kwa upande wake Balozi, anayemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini Mhe. Al Maliki ambaye amekuwa hapa nchini kwa kipindi cha miaka minne amesema anajisikia fahari na bahati kupata fursa ya kuiwakilisha nchi yake hapa Tanzania na kwamba katika kipindi chake chote amepata ushirikiano mkubwa.
“Kwa
kweli wakati wote wa uwakilishi wangu, nimekuwa nikipata ushirikiano wa kutosha
wakati wa kutekeleza majukumu yangu jambo hili limenifurahisha sana……........na
nitakuwa balozi mwema kwa Tanzania,” Amesema Balozi Al Maliki
Balozi
Al Maliki amewasihi watanzania kuendelea na utamaduni wao unaowafanya
kuheshimika duniani kote hususani katika suala la umoja, amani na mshikamano
bila ya kujali itikadi za kisiasa na dini.
Tanzania
na Saudi Arabia zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu katika sekta ya kilimo, elimu,
afya, biashara na uwekezaji, maji, utalii, kwa lengo la kuhakikisha utekelezaji
wa diplomasia ya uchumi unafikiwa kwa wakati.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge akiongea na Balozi wa Saudi Arabia hapa nchini, Mhe.
Mohamed Bin Mansour Al Maliki wakati balozi huyo alipokuwa anamuaga katika
ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi
wa Saudi Arabia hapa nchini, Mhe. Mohamed Bin Mansour Al Maliki akimueleza
jambo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar
es Salaam
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge akimkabidhi zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro Balozi
wa Saudi Arabia hapa nchini, Mhe. Mohamed Bin Mansour Al Maliki katika ofisi ndogo
za Wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi
wa Saudi Arabia hapa nchini, Mhe. Mohamed Bin Mansour Al Maliki akimkabidhi
zawadi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar
es Salaam
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.