Na Mwandishi wetu, Dar es
Salaam
Mabalozi
mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, ‘wamemlilia’ Makamu wa Kwanza
wa Rais Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad na kumuelezea kwa mema
aliyoyafanya enzi za uhai wake hapa duniani.
Mabalozi
hao wamewasili katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa nyakati
tofauti kwa ajili ya kusaini kitabu cha maombolezo ambapo mara baada ya kusaini
kitabu cha maombolezo baadhi yao wakaelezea walivyoguswa na msiba wa Mhe.
Maalim Seif Sharif Hamad.
Balozi
wa Ufaransa chini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier amesema kuwa ni pengo kubwa
kwa Zanziba na kwa Tanzania pia kwani Mhe. Maalim Seif alikuwa kiongozi mahiri
kwa taifa na aliyekuwa na uhamasisho kwa bara la Afrika.
“Alikuwa
mtetezi wa masuala mbalimbali ikiwemo demokrasia na haki, pia katika enzi za
uhai wake alikubali kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais kwa Serikali ya Zanzibar ni
jambo la kuigwa kwa taifa la Zanzibar na Taifa la Tanzania kwa Ujumla,” Amesema
Mhe. Clavier
Mhe.
Clavier ameongeza kuwa “Maalimu Seif alikuwa kiongozi aliyependa amani, na
aliyekuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya nchi yake……lakini pia alikuwa
mpenda amani na alikuwa mwanasiasa makini ……..kwa kweli tutamkumbuka daimia,
tunamuombea kwa Mungu apumzike kwa amani,”.
Kwa
upande wake Balozi wa Finland hapa nchini Mhe. Riitta Swan amesema kuwa Maalim
Seif Sharif Hamad alikuwa kiongozi makini aliyependa amani na mshikamano wakati
wa uhai wake.
“Kwa
muda mfupi niliomfahamu kwa kweli alikuwa kiongozi mahiri aliyependa amani na
umoja hakika pengo lake halitazibika kwa urahisi, Mungu ampumzishe kwa amani,”
Amesema Mhe. Swan
Nae Balozi wa Zimbabwe hapa nchini, Mhe. Luteni Jenerali Mstaafu, Anselem Sanyatwe amesema kuwa Mhe. Maalim Seif alikuwa ni kiongozi mchapakazi na mzalendo kwa taifa la Zanzibar na Tanzania. “Kwa kweli Jamhuri ya MUungano imepoteza kiongozi mzalendo, kwa niaba ya Jamhuri ya Zimbabwe natoa pole kwa Tanzania kwa kuondokewa na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar…..poleni sana watanzania kwa msiba huu mzito,” Amesema Mhe.
Kwa
upande wake Balozi wa Kuwait nchini, Mhe. Balozi Mubarak Mohammed Alsehaijan amesema
kuwa Mhe. Maalim Sief kiongozi mpenda amani na atakumbukwa daima kwa mema
aliyoyafanya kwa Wazanzibari na watanzania kwa ujumla.
Baadhi
ya mabalozi waliofika na kusaini kitabu cha maombolezo katika Ofisi Ndogo za
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam
ni pamoja na Balozi wa Zambia nchini mhe. Benson Keith Chali, Balozi wa Finland
chini Tanzania, Mhe. Riitta Swan na Balozi wa Kuwait nchini, Mhe. Balozi
Mubarak Mohammed Alsehaijan.
Wengine
ni Balozi wa Pakistani hapa nchini, Mhe. Mohammad Saleem, Balozi wa Ufaransa
hapa chini, Mhe. Frederic Clavier, Balozi wa Zimbabwe hapa nchini, Mhe. Luteni
Jenerali Mstaafu, Anselem Sanyatwe pamoja na Mwakilishi wa Balozi wa Irani hapa
nchini. Bwn. Mohammad Rezaee.
Balozi
wa Ufaransa chini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier akisaini kitabu cha
maombolezo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki kufuatia kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mhe. Maalim
Seif Sharif Hamad jijini Dar es Salaam
Balozi
wa Finland hapa nchini, Mhe. Riitta Swan akisaini kitabu cha maombolezo katika
Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kufuatia
kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad jijini
Dar es Salaam
Balozi
wa Kuwait hapa nchini, Mhe. Balozi Mubarak Mohammed Alsehaijan akisaini kitabu
cha maombolezo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki kufuatia kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mhe. Maalim
Seif Sharif Hamad jijini Dar es Salaam
Balozi
wa Zimbabwe hapa nchini, Mhe. Luteni Jenerali Mstaafu, Anselem Sanyatwe akisaini
kitabu cha maombolezo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki kufuatia kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar,
Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad jijini Dar es Salaam
Balozi
wa Pakistani hapa nchini, Mhe. Mohammad Saleem akisaini kitabu cha maombolezo
katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
kufuatia kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif
Hamad jijini Dar es Salaam
Mwakilishi
wa Balozi wa Irani hapa nchini. Bwn. Mohammad Rezaee kitabu cha maombolezo
katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
kufuatia kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif
Hamad jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.