Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika unatarajiwa kufanyika tarehe 3 na 4 Februari, 2021 kwa njia mtandao (video conference).
Mkutano huo pamoja na mambo mengine utaandaa rasimu ya agenda za Mkutano wa 34 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika utakaofanyika tarehe 6 na 7 Februari, 2021.
Mkutano huo utajadili
na kupitisha mapendekezo ya taarifa ya Mkutano wa 41 wa Kamati ya Kudumu ya
Uwakilishi (Permanent Representatives
Committee –PRC),taarifa ya hali ya ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (COVID-19) Barani Afrika na taarifa ya
Mkutano wa Pamoja wa Kamati ya Baraza la Mawaziri ya Tathimini na Kamati ya
Mawaziri 15 wa Fedha.
Mkutano pia
utafanya uchaguzi na Uteuzi wa Wajumbe Sita (6) wa Bodi ya Ushauri ya Masuala
ya Rushwa ya Afrika, Makamishna wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Majaji wanne
(4) wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.