Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi na ujumbe wa Tanzania wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa 38 wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika unaofanyika kwa njia ya video.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akifuatilia ufunguzi wa Mkutano huo unaofanyika kwa njia ya video.
Mkutano wa Kawaida wa Baraza la
Mawaziri wa Umoja wa Afrika unaofanyika kwa njia video (video conference) umeanza.Mkutano huo umefunguliwa na Mwenyekiti wa
Baraza la Mawaziri la Umoja huo na Waziri wa Ushirikiano na Uhusiano wa
Kimataifa wa Afrika Kusini Mhe. Dkt. Naledi Pandor
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi ameongoza ujumbe wa Tanzania kutokea katikaa mji wa Serikali Mtumba ulioko Makao Makuu ya nchi jijini Dodoma.
Mkutano huo wa kawaida wa siku mbili unaongozwa na Mwenyekiti wa
Baraza hilo Mhe. Dr. Naledi Pandor Waziri wa Ushirikiano na Uhusiano wa
Kimataifa wa Afrika Kusini pamoja na mambo mengine utaandaa rasimu ya agenda za
Mkutano wa 34 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika
utakaofanyika tarehe 6 na 7 Februari, 2021 kwa njia video
Mkutano huo unajadili na kupitisha mapendekezo ya taarifa ya
Mkutano wa 41 wa Kamati ya Kudumu ya Uwakilishi (Permanent Representatives Committee –PRC),taarifa ya hali ya
ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (COVID-19)
Barani Afrika na taarifa ya Mkutano wa Pamoja wa Kamati ya Baraza la Mawaziri
ya Tathimini na Kamati ya Mawaziri 15 wa Fedha.
Mkutano
pia utafanya uchaguzi na Uteuzi wa Wajumbe Sita (6) wa Bodi ya Ushauri ya
Masuala ya Rushwa ya Afrika, Makamishna wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika na
Majaji wanne (4) wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.