Na Mwandishi wetu,
Serikali
ya Ufaransa imeahidi kutoa Euro milioni 150 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 413 kwa ajili
ya kuendeleza mradi wa awamu ya tano wa ujenzi wa mradi wa mabasi ya mwendokasi
jijini Dar es Salaam.
Ahadi
hiyo imetolewa na Balozi wa Ufaransa hapa nchini, Mhe. Frederic Clavier wakati
alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi, (Mb) katika ofisi ndogo za Wizara
jijini Dar es Salaam.
Prof.
Kabudi amesema kuwa mazungumzo yake na Mhe. Clavie yalijikita katika
utekelezaji wa mambo waliyokubaliana wakati alipofanya ziara ya kikazi mwezi
Februari nchini Ufaransa.
“Leo
katika mazungumzo yangu mimi na Mhe. Balozi tumejadili mambo mbalimbali
likiwemo suala la Shirika la Maendeleo la Ufaransa kutoa fedha kwa ajali ya kuendeleza
mradi wa awamu ya tano wa ujenzi wa mradi wa mabasi ya mwendokasi jijini Dar es
Salaam,” Amesema Prof. Kabudi
Pamoja
na mambo mengine, Prof. Kabudi amesema kuwa wamejadili kuhusu miradi ya
maendeleo katika sekta ya nishati, maji, afya na kilimo.
“Pia
tumejadili kuhusu ushiriki wa Ufaransa katika kuisaidia Tanzania katika uchumi
wa buluu, ambapo Shirika la Maendeleo la Ufaransa limeahidi kusaidia Tanzania
bara na Zanzibar katika kuendeleza uchumi wa buluu na hasa kuongeza uwezo wa
Tanzania kuvua na kuchakata samaki,” Ameongeza Prof. Kabudi.
Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa Nchini, Mhe. Frederic Clavier amesema kuwa kikao chake na Mhe. Waziri ni mwanzo wa hatua mpya ya ushirikiano kati ya Tanzania na Ufaransa.
“Nchi
ya Tanzania ni nchi ya demokrasia na amani,ambapo inatoa fursa ya kuwekeza
katika miradi ya maendeleo, Ufaransa itaendelea kuwa pamoja na Tanzania katika
kuhakikisha kuwa inasonga mbele kimaendeleo,” Amesema Balozi Clavie
Katika
tukio jingine Prof. Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Umoja
wa Ulaya hapa nchini, Mhe. Manfredo Fanti na kujadili mambo mbalimbali ya
kuboresha ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya na Tanzania hasa kufuatia utiaji
saini wa miradi sita itakayopata uhisani wa fedha kutoka Umoja wa Ulaya.
“Tumekubaliana
kuimarisha uhusiano wetu katika maeneo mbalimbali ikiwemo, maeneo ya viwanda,
na kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara Tanzania, katika masuala ya
mabadiliko ya tabia nchi, kilimo, maji, miundombinu katika kuhakikisha kuwa
Tanzania inaongeza uwezo wake wa kuazilisha Nnishati.
Kwa upande wa, Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Fanti amesema kuwa pamoja na mambo mengine, wamejadili mambo ya kuboresha uhusiano wa kidiplomasia uliopa baina Umoja wa Ulaya na Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkaribisha Balozi wa Ufaransa
hapa nchini, Mhe. Frederic Clavier wakati walipokutana kwa mazungumzo katika
Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimuelezea jambo Balozi wa Ufaransa hapa nchini, Mhe. Frederic Clavier wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Mhe. Manfredo Fanti akimuelezea jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.