Na Mwandishi wetu, Dar
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameendelea
kumuamini Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge katika nafasi ya Katibu Mkuu Wizara
ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Balozi
Ibuge aliteuliwa Februari 06, 2020 kuwa katibu mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
ushirikiano wa Afrika Mashariki nafasi anayoendelea kuishikilia mpaka sasa.
Kabla
ya wadhifa huo, Balozi Ibuge alikuwa Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocal) Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Pia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuapisha
Balozi Fatma Mohammed Rajab kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Balozi Fatma aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Qatar Desemba 03, 2016 nafasi aliyokuwa akiishikilia hadi alipoteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (Hayupo Pichani)
akimuapisha Balozi Fatma Mohammed Rajab kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki leo Ikulu Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mhe. Balozi Fatma Mohammed Rajab wakipokelewa na baadhi ya watumishi katika Ofisi Ndogo za Wizara leo Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mhe. Balozi Fatma Mohammed Rajab mara baada ya kuwasili katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Fatma Mohammed Rajab akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Wizara wakati wa mapokezi katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.
Balozi Fatma Mohammed Rajab akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.