Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajab leo amewasili katika Ofisi za Makao Makuu ya Wizara zilizopo katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma na kupolewa na Watumishi na Menejimenti ya Wizara.
Balozi Fatma Rajab baada ya mapokezi hayo alipata wasaha wa kuongea na Wakuu wa Idara na Vitengo ambapo licha yakuwataka kuendelea kufanya kazi kwa weledi na juhudi amewaahidi ushirikiano katika kuteleza majumu yao ya kila siku.
Balozi Fatma aliapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki tarehe 6 Aprili, 2021.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajab akipokelewa Wizarani Mtumba, jijini Dodoma. |
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajab akisalimiana na Balozi Anisa Mbega alipowasili Wizarani. |
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajab akisalimiana na Balozi Stephen P. Mbundi wakati anapokelewa Wizarani. |
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajab akisaini kitabu cha wageni alipowasili Wizarani |
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajab akiongea na Watumishi na Menejimenti ya Wizara (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili Wizarani |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.