Na Mwandishi wetu, Dar
Aliyekuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ambae kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
amekabidhi Ofisi kwa Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo Mhe. Balozi Joseph Edward
Sokoine
Makabidhiano ya ofisi yameshuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb).
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki Balozi Joseph Sokoine
akipokea ua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati walipokuwa
wanamkaribisha katika Ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali watu, Bw. Alex Mfungo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki Balozi Joseph Sokoine
akiswasalimia baadhi ya wafanyakazi wa wizara katika Ofisi ndogo za wizara Jijini
Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb)
akimkabidhi ua Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki
Balozi Joseph Sokoine mara baada ya kuwasili katika Ofisi ndogo za wizara Jijini
Dar es Salaam kwa makabidhiano ya Ofisi. Kushoto ni aliyekuwa Katibu Mkuu
Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb)
akisalimiana na aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo Balozi Brigedia Jenerali
Wilbert Ibuge katika Ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki Balozi Joseph Sokoine.
Aliyekuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akimkabidhi ofisi Katibu Mkuu mpya Balozi
Joseph Sokoine. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za wizara Jijini
Dar es Salaam.

Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge na Katibu Mkuu mpya Balozi Joseph Sokoine wakiwa
wameshikana mikono mara baada ya kukabidhiana ofisi
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.