Na Mwandishi wetu
Pakistan na Iran zimeahidi kuendelea kuimarisha diplomasia ya uchumi na Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa maslahi mapana ya pande zote.
Ahadi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti wakati Mabalozi wa Pakistan
na Iran walipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika Ofisi ndogo za
Wizara jijini Dar es Salaam.
Mabalozi waliokutana na Waziri Mulamula ni Balozi wa Pakistani
hapa nchini Mhe. Mohammad Saleem pamoja na Kaimu Balozi wa Irani hapa nchini
Mhe. Hossein Alvandi Behineh ambapo viongozi hao wamejadili masuala ya
kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Nchi zao lakini pia kuimarisha na
kuboresha diplomasia ya uchumi kwa maslahi mapana ya nchi zote.
Pamoja na mambo mengine, Balozi wa Pakistan Mhe. Saleem ameelezea
kufurahishwa na uhusiano mzuri uliopo baina ya Iran na Tanzania na amepongeza
hatua mbalimbali ambazo Serikali ya Tanzania imeendelea kuzichukua katika
kuimarisha diplomasia ya uchumi.
Nae Kaimu Balozi wa Iran amesisitiza juu ya uwekezaji na biashara
ambapo amesema kuwa Serikali yake ipo tayari kufanya biashara na Tanzania na
kuinua uchumi wa wananchi wan chi zote mbili.
Kwa upande wake Balozi Liberata Mulamula (Mb) amewahakikishia
mazingira salama ya biashara na uwekezaji na kuwaahidi ushirikiano wa kutosha
kutoka Tanzania.
Kadhalika, Waziri Mulamula amesema ushirikiano wa diplomasia ya uchumi kati ya Tanzania na Pakistan unatoa fursa nyingi ikiwemo kukuza biashara hasa katika sekta ya kilimo ikiwemo chai, pamba, korosho, mbegu za mafuta, Madini ya Tanzanite, pamoja na uwekezaji.
Kikao kikiendelea |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.