Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo, ametembelea Ubalozi wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini.
Jenerali Mabeyo yupo Nchini Afrika Kusini kuhudhuria sherehe za kumuaga Mkuu Majeshi wa Afrika Kusini Jenerali SZ Shoki zilizofanyika kitaifa Jana Mjini Pretoria. Kuhudhuria sherehe hizi,ni utaratibu uliowekwa na nchi wanachama wa Jumuiya za SADC ya maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika kuimarisha mashirikiano hususan katika nyanja ya Diplomasia ya Ulinzi (Defence Diplomacy) na Amani katika eneo Ia nchi za SADC.
Jenerali Mabeyo, alikaribishwa Ubalozini na Mhe. Balozi Mej. Jen.
Gaudence Milanzi (Mst) na watumishi wa Ubalozi Mhe. Balozi Milanzi alitoa taarifa
fupi ya eneo la uwakilishi ya Afrika Kusini, Botswana na Falme ya Lesotho.
Mhe. Balozi alieeza kuwa hali ya uwakilishi inaridhisha kiulinzi
na kiusalama, Ubalozi umeendelea kukuza mashirikiano na nchiza eneo la uwakilishi
ikiwa ni pamoja na SADC. Kwa kufuata miongozo ya sera ya Mambo ya Nje ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania inavyoelekeza kuendeleza Diplomasia ya kisiasa na kutekeleza
Diplomasia ya uchumi.
Upande wake Jenerali Mabeyo alielezea ziara yake kwa ujumla nchini
Afrika Kusini imekuwa ni ya mafanikio, na pia kuna mambo kama ambayo kama Mkuu wa Majeshi ameona yanafaa kuigwa ili kuboresha
utendaji wa Jeshi la Tanzania.
Jenerali Mabeyo amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan, amelenga
kuendeleza maendeleo ndani na nje ya nchi mfano katika kutekeleza Sera ya Mambo
ya Nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na mwelekeo unaelekeza kuimarisha Diplomasia kwa kujenga mahusiano na nchi duniani kwa kuimarisha
Diplomasia ya siasa na Diplomasia ya uchumi.
Jenerali Mabeyo alimsihi Balozi na watumishi wa Ubalozi kuhakikisha
kuwa wanaielewa na kuisimamia dira ya Diplomasia kama ilivyoainishwa na Mhe. Rais
Samia Suluhu Hassan, ili kuweza kutelekeza majukumu yao kwa wepesi.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania
(CDF) Jenerali Venance Mabeyo akimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Afrika
Kusini Mhe. Meja Jenerali (Mst) Gaudence Milanzi wakati alipotembelea ubalozi
huo Jijini Pretoria
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania
(CDF) Jenerali Venance Mabeyo akiwa kwenye kikao na Balozi wa Tanzania nchini
Afrika Kusini Mhe. Meja Jenerali (Mst) Gaudence Milanzi pamoja na watumishi wa
Ubalozi wakati alipotembelea ubalozi huo Jijini Pretoria
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania
(CDF) Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa
Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe. Meja Jenerali (Mst) Gaudence Milanzi pamoja
na watumishi wa Ubalozi
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.