Na Mwandishi wetu,
Dar
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imesema Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika viwango vya Utawala Bora na Haki za Binadamu hususani katika maeneo ya haki za kijamii pamoja na haki za kisiasa.
Mwenyekiti wa Tume hiyo (Jaji Mstaafu) Mathew Mwaimu ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) na kuongeza kuwa licha ya uwepo wa baadhi ya maeneo ya maboresho kwa sasa Tanzania iko katika daraja “A” miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika masuala ya Utawala Bora na Haki za Binadamu.
“Licha ya uwepo wa baadhi ya maeneo ya maboresho kwa
sasa Tanzania iko katika daraja “A” miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika
masuala ya Utawala Bora na Haki za Binadamu,” amesema Jaji Mwaimu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameipongeza Tume hiyo kwa kutekeleza
majukumu yake ikiwemo kuishauri Serikali katika kuzingatia na kutekeleza
masuala ya haki za binadamu na utawala bora kama ilivyoridhia katika majukwaa
ya kimataifa.
“Naipongeza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
kwa kutekeleza majukumu yake vizuri ikiwemo kuishauri Serikali katika
kuzingatia na kutekeleza masuala ya haki za binadamu na utawala bora kama
ilivyoridhia katika majukwaa ya kimataifa,” amesema Balozi Mulamula.
Balozi Mulamula ameongeza kuwa Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora ya Tanzania ni mwanachama katika tume nyingine za
kikanda na kimataifa ambazo hupima viwango vya utekelezaji wa Haki za binadamu
na Utawala Bora ambapo kwa sasa Tanzania ina kiwango “A”.
Mwenyekiti
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (Jaji Mstaafu) Mathew Mwaimu
akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Balozi Liberata Mulamula wakati walipokutana kwa maongezi katika ofisi ndogo za
Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiteta
jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (Jaji Mstaafu)
Mathew Mwaimu wakati walipokutana kwa maongezi katika ofisi ndogo za Wizara Jijini
Dar es Salaam
Mazungumzo
baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Liberata Mulamula na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (Jaji
Mstaafu) Mathew Mwaimu yakiendelea katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es
Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika
picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (Jaji
Mstaafu) Mathew Mwaimu, Kamishna kutoka Tume ya haki za Binadamu na Utawala
Bora Bw. Nyanda Shuli na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.