Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiangalia zawadi iliyotolewa na wawakilishi wa Jumuiya ya St. Egidio ya nchini Italia walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 25/06/2021. |
mazungumzo yakiendelea |
Mmoja wa wawakilishi wa Jumuiya ya St. Egidio ya nchini Italia Bw. Andrea Bartoli akizungumza wakati wawakilishi hao walipomtembelea Balozi Mulamula ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 25/06/2021 |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na
wawakilishi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ya nchini Italia.
Katika mazungumzo hayo wawakilishi wa Jumuiya hiyo wakiongozwa
na Bw. Andrea Bartoli wamemuhakikishia Mhe. Waziri Mulamula kuwa Jumuiya yao
itaendelea na kazi ya kuhakikisha amani inatamalaki katika nchi mbalimbali barani
Afrika ikiwemo Tanzania.
Akizungumza nao Mhe. Waziri amewahakikishia wawakilishi hao
kwamba Tanzania itaendelea kuwaunga mkono katika harakati zao za kuwa na jamii
salama kwani kufanya hivyo kunasaidia dunia kuwa salama.
Amewaomba kuendelea na kazi ya kuifahamisha jamii juu ya kazi
zinazofanywa na Jumuiya hiyo katika sehemu mbalimbali nchini na barani Afrika
kwa ujumla.
Jumuiya hiyo inajihusisha na masuala ya utafutaji wa amani
kwa njia ya midahalo na mazungumzo ikiwa ni pamoja na kutoa misaada ya kijamii
katika jumuiya mbalimbali nchini na katika Bara la Afrika.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.