Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Liberata Mulamula mara baada ya kuzindua Baraza hilo jijini Dodoma tarehe 25/06/2021. |
wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya pamoja na Mhe. Waziri Mulamula |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amezindua Baraza jipya la Wizara na kuwataka
wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara kuwa mabalozi wazuri wa watumishi wa
Wizara wanaowawakilisha.
Mhe. Waziri Mulamula ametoa rai hiyo jijini Dodoma alipokuwa
akizindua Baraza hilo jijini Dodoma baada ya baraza la awali kumaliza muda
wake.
Amesema kwamba uongozi wake kwa kushirikiana na watendaji
wengine wa Wizara wako tayari kuyasikiliza na kuyafanyia kazi mapendekezo
watakayoyapeleka kwa uongozi wa Wizara na kuwataka kuyafanyia kazi mapendekezo
yanayotolewa na wafanyakazi ili yaweze kushughulikiwa.
Mhe. Waziri pia amewaambia wajumbe wa Baraza hio kwamba
uongozi wake hautovumilia tabia au vitendo vya utovu wa nidhamu kama vile
rushwa vitakavyolalamikiwa kufanywa na watumishi wa Wizara dhidi ya watu
wanaowahudumia.
Amesema ni matarajio yake kwamba watumishi wa Wizara watakuwa
waadilifu na wenye tabia njema wanapowahudumia wadau mbalimbali wa Wizara na
hivyo kutekeleza majukumu yao kwa kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni za
Utumishi wa Umma na hivyo kutekeleza majukumu ya wizara ipasavyo.
Amesema kuwa Wizara imejipanga kuhakikisha inatoa vifaa na
vitendea kazi kwa watumishi wake ili kuhakikisha utekelezaji wa majukumu ya
Wizara unakamilika na kuwa na ufanisi.
Kikao hicho cha Baraza kiliwapitisha wajumbe wake katika
mpango wa Bajeti wa mapato na matumizi ya wizara iliyopitishwa na Bunge mapema
mwezi huu, kiliwachagua Bibi Judica Nagunwa kuwa Katibu na Bw. Hassan Mnondwa
kuwa katibu Msaidizi wa Baraza hilo jipya ambalo litakaa madarakani kwa muda wa
miaka mitatu.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.