Na Mwandishi wetu, Dar
Serikali
ya Tanzania inategemea kunufaika na soko la bidhaa zake katika masoko ya nje
baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa ushiriki katika Eneo Huru la Biashara barani
Afrika (AfCFTA).
Akiongea
na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Katibu
Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCTA) Mhe. Wamkele
Mene, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Liberata Mulamula (Mb) amesema kwa sasa Serikali ipo katika hatua za mwisho
kusaini Mkataba wa AfCTA.
“Lengo
la ziara ya Mhe. Mene hapa nchini pamoja na mambo mengine ni kukutana na
viongozi na wadau wengine muhimu kujadiliana na masuala mbalimbali yanayohusu
Mkataba wa AfCTA ikiwa ni pamoja na umuhimu wa Tanzania kuridhia Mkataba huo,”
Amesema Balozi Mulamula
Balozi
Mulamula ameongeza kuwa, uanzishwaji wa AfCTA ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa
ambapo pamoja na mambo mengine, utekelezaji wake unatarajiwa kuongeza wigo wa
fursa nafuu za biashara nchini kwa kuwavutia wawekezaji na kuongeza mauzo hasa
ya bidhaa za kilimo.
Kwa
upande wake, Katibu Mtendaji wa Sekretariati ya Eneuo Huru la Biashara Afrika (AfCTA)
Mhe. Wamkele Mene ameishukuru Tanzania kwa ushirikiano ambao imempatia tangu
wakati wa uchaguzi hadi sasa na kuahidi kuwa utekelezaji wa Mkataba huo
utanufaisha kila Nchi Mwanachama.
“……….Naipongeza
Serikali ya Awamu ya Sita kwani tangu ilipoingia Madarakani imetumia muda mfupi
katika kushiriki kwa ukamilifu katika majadiliano ya kusaini mkataba huu na
Tanzania imeshiriki vizuri sana kwenye majadiliano haya muhimu,” Amesema Mhe.
Wene
Ameongeza
kuwa kwa sasa Eneo Huru la Biashara Afrika lina Nchi wanachama 38 ambazo
zimekubaliana na Mkataba huo na kwamba kwa sasa Sekretariati hiyo inaendelea
kuimarika katika kukuza biashara na sekta binafsi katika nchi wanachama wa AfCTA.
Mkataba
wa Eneo Huru la Biashara Afrika umesainiwa na Nchi 54 kati ya nchi 55 za Umoja
wa Afrika ikiwemo Tanzania. mkataba huo ulipata nguvu ya Kisheria Julai, 2019
baada ya nchi 28 kuridhia Mkataba huo. Mkataba wa AfCTA unahusisha maeneno ya
ushirikiano katika bishara ya bidhaa, biashara ya huduma, uwekezaji, hakimiliki
na ubunifu pamoja na Sera za ushindani.
Katika
tukio jingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Liberata Mulamula (Mb) ameshiriki uzinduzi wa Kongamano la Usawa wa Kijinsia
ambapo pamoja na mambo mengine, Balozi Mulamula kongamano hili litakuwa mahsusi
kuangalia masuala ya uswa wa jinsia kwa kizazi hiki na kizazi kijacho na kwamba
wakuu wa Nchi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa watakuatana Ufaransa katika
kongamano hilo kuanzia tarehe 30 Juni hadi 2 Julai 2021.
Balozi
Mulamula ameongeza kuwa, Tanzania itashiriki katika kongamano hilo ambapo Rais
wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan atawakilishwa na Makamu wa Rais
Mhe. Dkt. Philip Mpango
Uzinduzi
wa Kongamano la Usawa wa Kijinsia uliofanyika leo jijini Dar es Salaam umehudhuriwa
na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Fredric Clavie pamoja na Mwakilishi kutoka
Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Bibi Hodan Addou.
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiongea
na waandishi wa Habari wakati alipokutana na Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya
Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) Mhe. Wamkele Mene leo Jijini Dar es
Salaam
Katibu
Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) Mhe. Wamkele
Mene akiongea na waandishi wa Habari wakati wa Mkutano baina yake na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb)uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam
Katibu
Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) Mhe. Wamkele
Mene akiongea na waandishi wa Habari wakati wa Mkutano baina yake na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb)uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam
Mkutano
ukiendelea
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb) akihutubia wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Usawa wa Kijinsia ulifanyika
Jijini Dar es Salaam
Balozi
wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Fredric Clavie akihutubia wakati wa uzinduzi
wa Kongamano la Usawa wa Kijinsia ulifanyika Jijini Dar es Salaam
Mwakilishi
kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Bibi Hodan Addou akihutubia wakati wa uzinduzi
wa Kongamano la Usawa wa Kijinsia Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb), Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Fredric Clavie pamoja na Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Bibi Hodan Addou wakiwa katika picha ya
pamoja
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.