Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mkurugenzi
wa Kitengo cha wa Diaspora Balozi Anisa Mbega akizungumza kuwakaribisha Wanafunzi
wa kozi ya Astashahada ya uzamili kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) na wakufunzi
wao waliotembelea Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa ajili ya kujifunza
Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi
akizungumza baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati ya Wanafunzi wa kozi ya Astashahada
ya uzamili kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) na wakufunzi wao waliotembelea Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa ajili ya kujifunza
Wanafunzi wa kozi ya Astashahada ya uzamili kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) na wakufunzi wao wamefanya ziara ya mafunzo kwa kutembelea Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma na kuzungumza na watendaji wa Wizara kwa ajili ya kujifunza namna Wizara watendaji wa Wizara wanavyotekeleza diplomasia ya uchumi kupitia kazi zao.
Wanafunzi hao kutoka kampasi ya Dar es Salaam na Dodoma walipata nafasi ya kusikiliza mada za muundo na majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001.
Akizungumza wakati wa kuwakaribisha wanachuo hao kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mkurugenzi wa Kitengo cha wa Diaspora Balozi Anisa Mbega aliwataka wanachuo hao kusikiliza kwa umakini mada zitakazotolewa na watendaji wa Wizara ambao wanafanya shughuli za kidiplomasia kwa vitendo ili kujiongezea ujuzi zaidi.
Balozi Anisa aliwaambia wanachuo hao kuwa Wizara inaona fahari kuwa na chuo hicho kwani kinawezesha upatikanaji wa elimu ya diplomasia kwa wananchi wengi na kuwataka wanachuo hao kuitumia elimu wanayoipata kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla
Akizungumza kukamilisha mazungumzo kati ya wanachuo hao na watendaji wa Wizara Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Balozi Stephen Mbundi aliwataka wanachuo hao kuwa tayari na kujiandaa na dunia ya sasa ili waende na wakati uliopo na aliwaahidi kuwa Wizara iko tayari muda wowote kuwasaidia ili waweze kuitendea haki elimu waliyoipata.
Wanachuo hao na wakufunzi wao walikuwa na ziara ya siku mbili jijini Dodoma ambapo siku ya kwanza walienda kutembelea Bunge kwa mwaliko wa Naibu Waziri –Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Nassor Mbarouk na kujionea jisni Bunge la Tanzania linavyoendesha shughuli zake.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.