Na Mwandishi wetu, Dar
Mtandao
wa Uongozi wa Wanawake Afrika (AWLN) kwa kushirikiana na Taasisi ya Mwalimu
Nyerere umepewa changamoto ya kukuza na kusimamia masuala ya umoja na amani
katika Bara la Afrika ili kuleta maendeleo ya watu.
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ametoa
wito huo wakati alipokutana na Mtandao huo pamoja na Taasisi ya Mwalimu Nyerere
ikishirikiana na Shirika la Kimataifa la kutetea Haki na Maendeleo ya Wanawake
(UN Women) leo jijini Dar es Salaam
“Agenda
yetu ni muhimu, hamuwezi kusema kuwa tuna maendeleo kama hakuna amani…….amani
ni sehemu ya Diplomasia ya Uchumi, kama amani huwezi kuitafuta kwa njia
nyingine tuseme amani ni maendeleo na maendeleo ni amani,” Amesema Balozi
Mulamula
Balozi
Mulamula ameongeza kuwa, kwa kuzingatia kwamba amani ni matokeo ya haki juhudi
zinahitajika katika kuhamasisha na kuunga mkono ushiriki kamili wa wanawake
kama wadau muhimu wa kulinda na kutetea amani.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Bw. Joseph
Butiku amesema kuwa Taasisi yake ina jukumu la kuhakikisha kuwa amani na haki
zinapatikana hasa katika ukanda wa Maziwa Makuu.
“Tumepokea
changamoto tuliyopewa na Mhe. Waziri na mimi ninakubaliana na yeye kabisa kuwa
tushirikiane na wanawake katika kuhamasisha na kutunza amani na haki hasa kwa
kushirikiana na wanawake ambao wamekuwa na mchango mkubwa sana wa kutunza amani
na kuwa hakuna mpaka na yote yanawezekana,” Amesema Bw. Butiku.
Mtandao
wa Uongozi wa Wanawake Afrika (AWLN) na UN Women umekuwa ukishirikiana katika
kuisaidia Tanzania kuandaa Mpango kazi wa Kitaifa wa Utekelezaji wa ajenda ya
wanawake, amani na usalama ya Maamuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Na. 1325.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Bw. Joseph Butiku akimueleza jambo Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (wa
kwanza kulia), Mtandao wa Uongozi wa Wanawake Afrika (AWLN) pamoja na baadhi pamoja
na baadhi ya viongozi wa Shirika la Kimataifa la kutetea Haki na Maendeleo ya
Wanawake (UN Women) leo jijini Dar es Salaam
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiongea
na baadhi ya viongozi na maafisa wa Mtandao wa Uongozi wa Wanawake Afrika
(AWLN) pamoja na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (hawapo pichani) leo jijini Dar es
Salaam
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula
akiongea na baadhi ya viongozi na maafisa wa Mtandao wa Uongozi wa Wanawake
Afrika (AWLN) pamoja na Taasisi ya Mwalimu Nyerere leo jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na viongozi na maafisa wa Mtandao wa Uongozi wa Wanawake Afrika (AWLN) wafanyakazi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere pamoja na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.