Na Mwandishi wetu, Dar
Serikali
imewaeleza Mabalozi njia mbalimbali inazozitumia kudhibiti maambukizi ya virusi
vya corona ikiwa ni pamoja na kuridhia uingizwaji wa chanjo ya Uviko 19 kwa
Balozi, Taasisi na Mashirika ya Kimataifa yanayotaka kufanya hivyo.
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb)
amewaeleza baadhi ya Mabalozi wanaotoka katika nchi za Kiislamu wakati
alipokutana nao kwa ajili ya kuhitimisha sherehe za Eid El Haj leo jijini Dar
es Salaam.
Pia
Balozi Mulamula amefafanua kuhusiana na maswali aliyokuwa akiulizwa na baadhi
ya mbalozi juu ya chanjo ya kukabiliana na ugonjwa wa Uviko 19 na kusema kuwa
hakuna Balozi, Taasisi au Mashirika ya Kimataifa yalizuiliwa kuingiza chanjo
kwaajili ya kuwachanja watu wao na kuwasihi kutoa taarifa kwa wizara ya Afya
ili kuwezesha namna bora ya kuratibu na kupokea chanjo hizo.
“…….Naomba
niwahakikishie waheshimiwa mabalozi kuwa Serikali yetu ni sikivu sana, nimekuwa
nikiulizwa maswali mbalimbali kuhusu uingizwaji wa chanjo kwa ajili ya
kuwachanja watumishi katika balozi zenu hapa nchini ila naomba msisite
kuwasiliana na Wizara ya Afya kwa ajili ya kuratibu njia bora ya kupata chanjo
hiyo,” Amesema Balozi Mulamula.
Katika tukio
jingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Liberata Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Canada nchini
Mhe. Pamela O'Donnell pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar.
Balozi
Mulamula amekutana na mabalozi hao kwa nyakati tofauti katika Ofisi ndogo za
Wizara Jijini Dar es Salaam ambapo awali amekutana na Balozi wa Canada nchini,
Mhe. Pamela O'Donnell akifuatiwa na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David
Concar kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali ya uhusiano wa kidiplomasia
baina ya Tanzania na nchi zao.
Pamoja na
mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya kuendeleza na
kuimarisha ushirikiano wa uwili (Bilateral Cooperation).
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
akimsikiliza Balozi wa Palestina nchini, Mhe. Hamdi Mansour wakati alipokutana
na Mabalozi wanaotoka katika nchi za Kiislamu kwa ajili ya kuhitimisha sherehe
za Eid El Haj leo jijini Dar es Salaam
Balozi wa
Visiwa vya Comorro nchini, Mhe. Dkt. Ahmada El Badaoui Mohammed akimkaribisha
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata
Mulamula katika hafla kuhitimisha sherehe za Eid El Haj leo jijini Dar es
Salaam
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
akiongea na Mabalozi wanaotoka katika nchi za Kiislamu alipokutana nao kwa
ajili ya kuhitimisha sherehe za Eid El Haj leo jijini Dar es Salaam
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa
na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Fatma Mohammed Rajab pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Idara mbalimbali za Wizara wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaotoka
katika nchi za Kiislamu mara baada ya
kuhitimisha sherehe za Eid El Haj leo jijini Dar es Salaam
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza
na Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Pamela
O'Donnell wakati walipokutana kwa Mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara
jijini Dar es Salaam
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini Mhe. David Concar wakati
walipokutana kwa Mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.