Na Mwandishi wetu, Dar
Bunge
la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) limemuapisha Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula kuwa Mjumbe wa Baraza
la Maamuzi wa Bunge hilo.
Akizungumza
mara baada ya kuapishwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Martin Ngoga leo tarehe 6
Juni 2021 katika mkutano uliofanyika kwa njia ya Mtandao jijini Dar es Salaam Balozi
Mulamula amesisitiza umuhimu wa bunge hilo kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano
kutokana na umuhimu na matarajio ya
Wananchi kwa Bunge hilo.
Aidha
Balozi Mulamula amepongeza jitihada zinazofanywa na Bunge hilo kuendelea na
vikao vyake kwa njia ya mseto ikiwa ni pamoja na kukutana ana kwa ana ama kwa
njia ya mtandao licha ya changamoto ya uwepo wa ugonjwa wa UVIKO – 19 hali
inayoonesha dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi.
“Wananchi
wamekuwa na matarajio makubwa sana kupitia Bunge hili la Afrika Mashariki kiuweza
kuona faida na mambo mazuri yanayofanyika kupitia jumuiya hii ya Afrika
Mashariki,” Amesema Balozi Mulamula
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiapa
kuwa Mjumbe wa Baraza la Maamuzi wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) leo tarehe
6 Juni 2021 katika mkutano uliofanyika kwa njia ya Mtandao jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.