Na Mwandishi wetu, Dar
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango ameitaka Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Balozi za
Tanzania kuainisha na kutangaza fursa mbalimbali zilizopo nchini hususani
biashara na uwekezaji.
Dkt.
Mpango ametoa maelekezo hayo alipotembelea banda la Wizara ya Mambo ya nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki lililopo katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya
Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam. Mara
baada ya kuwasili katika banda la Wizara, Dkt. Mpango amepokelewa na Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor
Mbarouk.
“Naipongeza
Wizara kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya ya kuimarisha mahusiano ya
kidiplomasia ……..lakini pia Wizara iendelee kuzishirikisha Balozi zetu katika
kutangaza fursa mbalimbali zilizopo nchini, na Balozi hizo ziainishe fursa
mbalimbali zinazopatikana kwenye nchi za uwakilishi kwa ajili ya Watanzania,”
Amesema Dkt. Mpango
Pamoja
na mambo mengine, Dkt. Mpango ameielekeza Wizara ya Maambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuendelea kuboresha majukumu ya Wizara ikiwa ni
pamoja na balozi za Tanzania na Taasisi zake.
| Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiongea na
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Mbarouk Nassor Mbarouk pamoja na watumishi wa Wizara wakati alipotembelea banda
la Wizara katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika
viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam |
| Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiongea na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk pamoja na watumishi wa Wizara wakati alipotembelea banda la Wizara katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk
Nassor Mbarouk akisalimiana na watumishi wa Wizara wakati alipotembelea banda
la Wizara katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika
viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam | Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk
Nassor Mbarouk akisalimiana na watumishi wa Wizara wakati alipotembelea banda
la Wizara katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika
viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam |
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Geoffrey Mwambe (Mb) akipokea nakala ya
Jarida la Diplomasia linalochapishwa na
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipotembelea
banda la Wizara katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea
katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam | |
Afisa
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Ibrahim Mmbaga
akifafanua jambo kwa mwananchi aliefika kwenye banda la Wizara katika Maonesho
ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere
Dar es salaam
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.