Na Mwandishi wetu, Zanzibar
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuulinda Muungano kwa kuwa ndio
tunu kubwa ambayo imeachwa na waasisi wa Muungano huo na kwamba Serikali
haitotumia nguvu kwa baadhi ya wananchi wenye maoni taofauti bali
itawaelimisha.
Ahadi
hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla wakati
alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki ulioongozwa na Waziri wa Wizara hiyo Balozi Liberata Mulamula (Mb)
na kuongeza kuwa Zanzibar inatambua umuhimu wa Muungano uliopo pamoja na
manufaa yake huku akitolea mfano kwa baadhi ya Wazanzibar wanaoishi Bara ambao
ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe.
Hemed Suleiman Abdulla ameongeza kuwa kwa sasa Serikali imeweka kipaumbele katika
masuala ya kuimarisha uchumi na kuwaletea Wazanzibar maendeleo kutokana na
umoja, amani na mshikamano uliopo tangu uwepo wa muafaka wa Serikali ya Kitaifa
na kuwataka wafanyabiashara na wawekezaji kujitokeza kuwekeza visiwani humo
katika sekta mbalimbali ikiwemo eneo la Uchumi wa Buluu.
Akizungumza
wakati wa kujitambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kwa ushirikiano uliopo katika utendaji kazi na kwamba kwa sasa Wizara
inaendelea na maandalizi ili kuwawezesha Viongozi wakuu wa pande zote mbili
kushiriki kikamilifu katika mikutano ya Kimataifa.
Uongozi
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukiongozwa na
Balozi Liberata Mulamula ambaye ameambatana na Naibu Waziri Balozi Mbarouk
Nassor Mbarouk, Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine pamoja na Naibu Katibu Mkuu
Balozi Fatma Mohammed Rajab na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara hiyo uko
visiwani Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha kwa viongozi wakuu wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiongea na Uongozi wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati uongozi huo
ulipomtembelea Ofisini kwake Zanzibar. Uongozi wa Wizara umeongozwa na Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula,
Naibu Waziri Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk, Katibu Mkuu, Balozi Joseph
Sokoine, Naibu Katibu Mkuu, Balozi Fatma Mohammed Rajab pamoja na baadhi ya
wakurugenzi wa Idara na vitengo vya Wizara.
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimueleza
jambo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati
uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje ulipomtembelea Ofisini Kwake Zanzibar
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akisisitiza jambo kwa
Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati
uongozi huo ulipomtembelea Ofisini kwake Zanzibar. Uongozi wa Wizara umeongozwa
na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata
Mulamula, Naibu Waziri Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk, Katibu Mkuu, Balozi
Joseph Sokoine, Naibu Katibu Mkuu, Balozi Fatma Mohammed Rajab pamoja na baadhi
ya wakurugenzi wa Idara na vitengo vya Wizara.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika picha ya pamoja na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata
Mulamula na Naibu Waziri Balozi Mbarouk
Nassoro Mbarouk
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.