Na Mwandishi wetu, Dar
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya (EU) zimeahidi kuimarisha
ushirikiano kwa maslahi ya pande zote mbili.
Hayo
yamesemwa kwenye mkutano kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine na Balozi wa Umoja wa
Ulaya (EU) hapa nchini, Mhe. Manfredo Fanti, uliofanyika katika Ofisi Ndogo za
Wizara Jijini Dar es Salaam.
Balozi
Sokoine ameeleza kuwa Serikali ya Tanzania inaridhishwa na uhusiano mzuri uliopo
kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya ambao umepelekea kuzaa matunda yenye manufaa
kwa pande zote mbili. Aidha, ameahidi kuendelea kuimarisha uhusiano huo kwa
maslahi ya pande zote.
Kwa
upande wake, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa Nchini, Mhe. Manfredo Fanti
amesema Umoja huo utaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza
miradi mbalimbali ya maendeleo.
“Napenda
kukuhakikishia kuwa Umoja wa Ulaya utaendelea kushirikiana kwa ukaribu na
Tanzania kwa ajili ya kuleta maendeleo ya wananchi wake,” amesema Balozi Fanti.
Katika
tukio jingine, Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Joseph Sokoine pia amekutana kwa mazungumzo na Kaimu Balozi
wa China hapa Nchini Mhe. Xu Chen katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es
Salaam.
Pamoja
na mambo mengine, viongozi hao wawili walijadili masuala mbalimbali ya kuendeleza
na kuimarisha ushirikiano wa uwili (Bilateral Cooperation).
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph
Sokoine akiongea na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa nchini, Mhe. Manfredo
Fanti wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini
Dar es Salaam
Balozi
wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa nchini, Mhe. Manfredo Fanti akimuelezea jambo Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph
Sokoine wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini
Dar es Salaam
Mazungumzo
baina ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Joseph Sokoine na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa nchini, Mhe.
Manfredo Fanti yakiendelea
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph
Sokoine akimueleza jambo Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Xu Chen wakati
walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Kaimu
Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Xu Chen akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine wakati
walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mazungumzo
baina ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Joseph Sokoine na Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Xu Chen yakiendelea
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.