WAZIRI MKUU MSTAAFU WA ETHIOPIA AHAMASISHA KILIMO KAMA NJIA YA KUONDOKANA NA UMASIKINI NCHINI
Tanzania imetakiwa kuwekeza zaidi katika sekta ya kilimo ili kuifanya nguvu ya Tanzania kuingia katika uchumi wa kati ionekane kwa wananchi walio wengi kutokana na uwepo wa fursa ya eneo kubwa la ardhi yenye rutuba.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mapinduzi ya kijani Afrika yaani Allience for a Green Revolution in Afrika (AGRA) ambaye pia ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Mhe Hailemariam Dessalegn ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula Jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa Tanzania ina eneo kubwa lenye rutuba kwa kilimo cha zao lolote na hivyo endapo sekta hiyo itapewa kipaumbele njia muafaka ya kuwaondoa katika umasikini wananchi wake. Ameongeza kuwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ni mjumbe katika Taasisi hiyo ambayo imekuwa ikihamasisha kilimo kwa ajili ya usalama wa chakula lakini pia kilimo cha biashara kwa kuangalia miradi na mpango wa kitaifa wa uendelezaji wa kilimo na kwa hapa Tanzania Taasisi hiyo imesaidia katika upatikanaji wa mbegu bora,mafunzo,umwagiliaji pamoja na utoaji wa mitaji kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanawake katika sekta hiyo.
Katika tukio jingine Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mhe. Sheikh Shakhboot Bin Nahyan ambaye ni Mjumbe Maalum wa Mrithi wa Ufalme wa Abu Dhabi na Naibu Kamanda Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Umoja wa Abu Dhabi Mhe. Mohamed Bin Zayed Al Nahyan ambapo katika mazungumzo hayo wamegusia suala la ushirikiano katika usafiri wa anga,biashara na uwekezaji.
Balozi Mulamula ameongeza kuwa fursa za ushirikiano katika Nyanja za biashara na uwekezaji kati ya Nchi hizo mbili ni kubwa ambapo kwa sasa kikwazo ni ugonjwa wa UVIKO 19 na kwamba baada ya maradhi hayo kumalizika pande zote mbili zitakutana ili kuibua maeneo ya kuchochea ukuaji wa uchumi kwa haraka.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.