Na Mwandishi wetu, Dar
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amekutana na kufanya mazungumzo na mabalozi watatu wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Balozi Sokoine amekutana kwa nyakati tofauti na mabalozi hao ambao ni Balozi wa India hapa nchini Mhe. Binaya Pradhan, Balozi wa Algeria hapa nchini Mhe. Ahmed Djellal pamoja na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Anders Sjöberg.
Pamoja na Mambo mengine viongozi hao wamejadili masuala ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia ulipo baina ya Tanzania na mataifa hayo ambapo awali Balozi wa India Mhe. Pradhan ameahidi kuendeleza na kudumisha uhusiano mzuri uliopo baina ya India na Tanzania.
“Nimemhakikishia Katibu
Mkuu, Mheshimiwa Balozi Sokoine kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia uliopo
baina ya mataifa yetu kwa maslahi ya pande zote mbili katika sekta mbalimbali
ikiwemo Utalii, elimu, gesi, biashara na uwekezaji,” amesema Balozi Pradhan
Kwa upande wake, Balozi wa Algeria hapa nchini, Mhe. Djellal amesema kuwa mazungumzo yao yaligusia masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Algeria na Tanzania.
“Tumekubaliana kuendelea
kuimarisha diplomasia baina ya mataifa yetu kwa maslahi mapana……….na kwa
maendeleo ya wananchi wetu,” amesema Balozi Djellal
Nae balozi wa Sweden hapa nchini Mhe. Sjöberg amesema katika jitihada za kuendeleza uhusiano wa Sweden na Tanzania, Sweden itaendelea kushirikiana na Tanzania kuendeleza sekta mbalimbali kwa manufaa ya pande zote mbili.
Kwa upande wake, Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Sokoine
amewahakikishia mabalozi hao ushirikiano wa kutosha kutoka Tanzania.
Katibu Mkuu Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiongea
na Balozi wa India hapa nchini Mhe. Binaya Pradhan katika Ofisi Ndogo za Wizara
Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Algeria hapa
nchini Mhe. Ahmed Djellal akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine katika Ofisi Ndogo za
Wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Sweden nchini
Mhe. Anders Sjöberg akimueleza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine katika Ofisi Ndogo za
Wizara Jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.