Na Mwandishi wetu, Dar
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amemuaga
Balozi wa Oman nchini, Mhe. Ally Abdallah Almahruqi katika ambaye amemaliza
muda wake wa uwakilishi hapa nchini.
Balozi Mulamula
amempongeza Balozi Almahruqi kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kudumisha uhusiano
wa kidiplomasia kati ya Oman na Tanzania wakati wote wa uwakilishi wake hapa
nchini.
“Tanzania tunashukuru
zaidi kwa ushirikiano uliotuonesha wakati wote ulipokuwa hapa kama Balozi na
tunakuahidi kuudumisha na kuuendeleza ushirikiano huo kwa maslahi ya nchi zetu
mbili (Tanzania na Oman)," amesema Balozi Mulamula
Kwa upande wake
Balozi wa Oman aliyemaliza muda wake wa uwakili hapa Nchini Mhe. Ally Abdallah
Almahruqi ameishukuru Tanzania kwa ushirikiano alioupata wakati wote alipokuwa
akitekeleza majukumu yake.
“Nawashukuru sana kwa ushirikiano mlionipatia wakati wote niliokuwa hapa nikitekeleza majukumu yangu kama Balozi, hakika nilifarijika sana……….naahidi kuwa nitakuwa balozi mwema kwa Serikali ya Tanzania,” amesema Balozi Almahruqi
Pia Balozi
ameipongeza Tanzania kwa hatua inazochukua za kupambana na virusi vya korona ikiwemo
kuungana na mataifa mengine duniani kuchanja chanjo ya Ugonjwa wa Virusi vya
Korona, UVIKO-19.
Tanzania na Oman zimekuwa zikishirikiana katika
sekta mbalimbali ikiwemo uwekezaji katika madini, mafuta, gesi, kilimo,
usafirishaji, utalii pamoja na biashara.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.