Tuesday, November 23, 2021

BALOZI FATMA AFUNGUA MADHIMISHO WIKI YA VYAKULA VYA KIITALIANO

 Na Mwandishi wetu, Dar

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab amefungua Maadhimisho ya Wiki ya Dunia ya vyakula vya Kiitaliano (World Week of Italian Cuisine).

Akifungua maadhimisho hayo jana jioni Jijini Dar es Salaam, Balozi Fatma amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Italia katika kuhakikisha uhusiano uliopo baina yake unaendele kuimarika na kuwasihi kutumia maadhimisho hayo pamoja na mambo mengine, kutangaza vivutio vya utalii hapa nchini.

“Italia imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali yetu katika nyanja mbalimbali ikiwemo utalii, elimu, biashara na uwekezaji………..naomba niwahakikishie tutaendelea kushirikiana ili kukuza maendeleo kwa maslahi ya pande zote mbili,” amesema Balozi Fatma

Balozi Fatma ameongeza kuwa Italia imekuwa mstari wa mbele katika sekta ya utalii na kuwasihi kutumia madhimisho hayo pia kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo Tanzania.

Kwa upande wake Balozi wa Italia nchini, Mhe. Marco Lombardi amesema Italia itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kudumisha na kuendeleza ushirikiano wake wa muda mrefu.

“Kupitia maadhimisho haya naamini kuwa yatakuwa chachu ya kuhamasisha upikaji wa vyakula mbalimbali vizuri ambavyo kwa namna moja au nyingine vitatoa ajira kwa watanzania pamoja na kuongeza fursa za utalii hapa nchini,” amesema Balozi Lombardi.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akisalimiana na Balozi wa Italia hapa nchini, Mhe. Marco Lombardi mara baada ya kuwasili kwenye makazi ya Balozi kwa ajili ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Dunia ya vyakula vya Kiitaliano (WORLD Week of Italian Cuisine) Jijini Dar es Salaam


Balozi wa Italia hapa nchini, Mhe. Marco Lombardi akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab katika Maadhimisho ya Wiki ya Dunia ya vyakula vya Kiitaliano (WORLD Week of Italian Cuisine) Jijini Dar es Salaam


Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui akisalimiana na Balozi wa Italia hapa nchini, Mhe. Marco Lombardi pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akisalimiana na Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Mhe. Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed


Balozi wa Italia hapa nchini, Mhe. Marco Lombardi akiteta jambo na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui katika Maadhimisho ya Wiki ya Dunia ya vyakula vya Kiitaliano (WORLD Week of Italian Cuisine) Jijini Dar es Salaam


Balozi wa Finland hapa nchini, Mhe. Riitta Swan akiteta jambo na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Dk. Donald Wright katika Maadhimisho ya Wiki ya Dunia ya vyakula vya Kiitaliano


Sehemu ya Mabalozi pamoja na wananchi waliojitokeza katika Maadhimisho ya Wiki ya Dunia ya vyakula vya Kiitaliano jijini Dar es Salaam


Balozi wa Italia hapa nchini, Mhe. Marco Lombardi akihutubia Mabalozi pamoja na wananchi waliojitokeza katika Maadhimisho ya Wiki ya Dunia ya vyakula vya Kiitaliano jijini Dar es Salaam


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akiwasilisha hotuba yake kwa mabalozi na wananchi (hawapo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Dunia ya vyakula vya Kiitaliano


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akiteta jambo na Balozi wa Finland hapa nchini Mhe. Riitta Swan


Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamela O'Donnell akiteta jambo na Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe. Dkt. Donald Wright



 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.