Na Waandishi wetu, Dar
Serikali
imetoa wito kwa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na Wakuu wa Mashirika
ya Kimataifa kuunga mkono juhudi za kusaidia upatikanaji wa chanjo ya Uviko 19
kwa Watanzania.
Wito
huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Liberata Mulamula (Mb) alipokutana na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao
pamoja na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mulamula amewasihi mabalozi hao kuendelea kuungana na Serikali katika jitihada
za upatikanaji wa chanjo ya Uviko 19 ambapo amesema kuwa hadi sasa ni watanzania
milioni 1.5 wamechanjwa
“Ninawaomba
zaidi chanjo nyingine ili watanzania wote waweze kuchanja kwani mwamko wa
kuchanja kwa sasa hapa nchini umekuwa mkubwa,” amesema Balozi Mulamula
Pia
Waziri Mulamula amewahakikishia kuwa Tanzania inazingatia masula ya demokrasia,
utawala bora, utawala wa sheria pamoja na kuheshimu haki za binadamu.
Kwa
upande wake kiongozi wa Mabalozi nchini ambaye pia ni Balozi wa Visiwa vya
Comoro nchini Mhe. Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed amesema pamoja na mambo
mengine, vikao hivyo vimekuwa na manufaa makubwa katika utekelezaji wa majukumu
yao hapa nchini.
Nae
Waziri wa uchumi wa buluu Zanzibar Mhe. Abdalla Hussein Kombo amesema katika
mkutano huo, wamejadili agenda ya uchumi wa buluu ambayo ina vipaumbele vitano
ambavyo ni uvuvi na utamaduni, utalii, usafirishaji, usimamizi wa bahari pamoja
na nishati.
“Tumewaeleza
wenzetu mabalozi vipaumbele vyetu vya uchumi wa buluu na wameonesha nia ya
kushirikiana na sisi katika kuendeleza agenda yetu ya Uchumi wa buluu,” amesema
Mhe. Kombo
“Pia
tumewaeleza kuwa tumemaliza kupitia sera yetu ya uchumi wa buluu na sasa
tumeshatekelez mpango wa utekelezaji na sasa tunataka tuone namna gani sisi na
wao tunaweza kuanza kuitekeleza agenda yetu ya uchumi wa buluu,” ameongeza Mhe.
Kombo
Mkutano
huo umehudhuriwa pia na Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba (Mb), Waziri wa
Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) na Naibu
Waziri wa Madini Mhe. Prof. Shukrani Manya pamoja na Katibu Mkuu na Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb) akiongea na mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha
nchi na Taasisi zao hapa nchini katika kikao cha pamoja kilichofanyika Jijini
Dar es Salaam
Kiongozi
wa Mabalozi nchini ambaye pia ni Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Mhe. Dkt.
Ahmada El Badaoui Mohamed akiongea na mabalozi (hawapo pichani) katika kikao
cha pamoja kilichoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph
Sokoine akiongea na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha
nchi na Taasisi zao hapa nchini katika kikao cha pamoja kilichofanyika Jijini
Dar es Salaam
Sehemu
ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi na Taasisi zao hapa nchini wakifuatilia kikao
Sehemu
ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi na Taasisi zao hapa nchini wakifuatilia kikao
Sehemu
ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi na Taasisi zao hapa nchini wakifuatilia kikao
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.