Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Liberata Mulamula leo tarehe 08 Disemba 2021 amekutana kwa
nyakati tofauti na kufanya mazungumzo na Viongozi kutoka nchi mbalimbali ambao
wapo nchini kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania
Bara yatakayofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 09 Desemba 2021.
Miongoni mwa Viongozi aliokutana nao ni pamoja na
Rais Mstaafu wa Malawi, Mhe. Dkt. Joyce Banda, Waziri wa Mambo ya Nje wa
Msumbiji, Mhe. Veronica Macamo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Eswatini, Mhe. Seneta
Thulisile Dladla na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Mhe. Dkt. Vicent Biruta.
Katika mazungumzo yao, Mhe. Balozi Mulamula
amewakaribisha nchini viongozi hao na
kuwashukuru kwa kukubali mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Samia Suluhu Hassan wa kuja kushiriki maadhimisho hayo pamoja na wananchi
wa Tanzania. Kadhalika, viongozi hao wamekubaliana kuimarisha ushirikiano kati
ya nchi zao na Tanzania kwenye maeneo mbalimbali.
Rais Mstaafu wa Malawi, Mhe. Dkt. Joyce Banda akiwa
katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Liberata Mulamula jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Msumbiji, Mhe. Veronica Macamo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es
Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda,
Mhe. Dkt. Vicent Biruta katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.