Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati la Jumuiya ya Afrika
Mashariki umefunguliwa leo tarehe 8 Februari 2022 jijini Arusha, Tanzania
katika ngazi ya Wataalamu.
Mkutano huu utafanyika katika ngazi tatu ambapo umeanza na;
Mkutano Ngazi ya Wataalamu unaofanyika tarehe 8 hadi 9 Februari 2022,
utafuatiwa na Mkutano Ngazi wa Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 10 Februari
2022 na utamalizika kwa Mkutano Ngazi ya Mawaziri utaofanyika tarehe 11
Februari 2022.
Lengo la Mkutano huu ni kupitia na kuandaa
taarifa ya hali ya utekelezaji wa Maamuzi/Maagizo ya mikutano iliyopita; Hatua
iliyofikiwa hadi sasa katika sekta za Nishati Umeme, Nishati Mafuta, na Nishati
Jadidifu; pamoja na Utekelezaji wa Miradi/Programu mbalimbali za Kitaifa na
Kikanda ya Sekta za Nishati inayotekelezwa ndani ya
Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Ujumbe wa Tanzania katika
Mkutano Ngazi ya Wataalamu unaongozwa na Kamishna Msaidizi Maendeleo ya
Umeme kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Styden Rwebangila ambaye ameambatana
na Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota,
Mkurugenzi Idara ya Nishati na Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini
Zanzibar, Mhandisi Said H. Mdungi pamoja na maafisa wengine Waandamizi kutoka
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wenye dhamana katika sekta ya nishati.
Mkutano Ngazi ya Wataalamu
na Ngazi ya Makatibu Wakuu ni sehemu ya mikutano ya awali kwaajili ya
maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati la
Jumuiya ya Afrika Mashariki utaofanyika tarehe 11 Februari 2022.
Kushoto ni Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhandisi Mgeta Sabe na wajumbe wengine wa Tanzania wakifatilia majadiliano. |
Ujumbe wa Tanzania. |
Sehemu nyingine ya Ujumbe wa Tanzania. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.