Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula
akisalimiana na Rais wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi
Adesina alipowasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma akiwa
katika ziara ya kikazi ya siku tatu nchini.
Rais
wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina awasili jijini Dodoma akiwa katika ziara ya
kikazi ya siku tatu nchini. Katika uwanja wa ndege wa Dodoma Dkt. Adesina
amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Liberata Mulamula na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba.
Dkt.
Adesina yuko nchini kwa ziara ya siku tatu ambapo
tarehe 09 February 2022 atashiriki katika uzinduzi wa ujenzi wa barabara za
mzunguko zinazojengwa katika jiji la Dodoma utakaofanywa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Ujenzi
wa barabara hizo za mzunguko zenye urefu wa kilomita 112.3 unagharamiwa kwa
pamoja kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na benki hiyo. Ujenzi wa barabara hizo utalifanya jiji la Dodoma kuwa na barabara za aina yake katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.