Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Korea Mhe. Chung Eui-yong ameelezea kuwa Serikali ya nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara na reli, usafiri wa majini, kuendeleza kilimo, uchumi wa buluu, uvuvi katika bahari kuu na teknolojia ya habari na mwasiliano.
Waziri Chung ameeleza haya alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahriki Mhe. Balozi Liberata Mulamula ambaye yupo ziarani nchini Korea.
Vilevile, Waziri Mulamula na Mwenyeji wake Mhe.Chung Eui-yong katika mazungumzo yao wamejadili kuhusu kuendelea kudumisha uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliopo baina ya mataifa hayo rafiki. Vilevile wamekubaliana kuendelea kuibua maeneo mapya ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa manufaa ya pande zote mbili.
Waziri Mulamula akiwa nchini humo anatarijia atashiriki sherehe za maadhimisho ya miaka 30 ya uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea yatakayofanyika jijini Seoul tarehe 29 Aprili 2022. Tanzania na Korea zilianzisha uhusiano wa Kidiplomasia Aprili 29,1992.
Balozi wa Tanzania nchini Korea Mhe.Togolani Mavula akifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea |
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Caesar Waitara akifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea |
Mazungumzo yakiendelea |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.