Mkutano wa Dharura wa Kamati
ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini
mwa Afrika (Extra-Ordinary Ministerial Committee of the Organ) ambao utahusisha pia Jamhuri ya Msumbiji na Nchi
Zinazochangia Vikosi katika Misheni ya SADC iliyopo Msumbiji (SAMIM) utafanyika
Pretoria, Afrika Kusini tarehe 03 Aprili 2022.
Mkutano huo ambao umetanguliwa na Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu (Senior Officials meeting), unalenga pamoja na mambo mengine Kupokea na Kujadili Ripoti
ya Maendeleo ya Misheni ya SADC nchini Msumbiji (SAMIM) pamoja na Mapendekezo mbalimbali kutoka kwa
Makatibu Wakuu.
Itakumbukwa kuwa, wakati wa Mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC ulichofanyika jijini Maputo,
Msumbiji mwezi Juni 2021, uliridhia kupelekwa kwa Misheni ya SAMIM (SADC
Mission in Mozambique) nchini Msumbiji kwa ajili ya kuisaidia nchi hiyo
kupamabana na ugaidi na vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake na watoto
vilivyokuwa vinaendelea kwenye baadhi ya Wilaya zilizopo kwenye Jimbo la Cabo
Delgado.
Misheni hiyo ambayo ilianza
kazi rasmi mwezi Julai 2021, inajumuisha Nchi Wanachama kumi (10) za SADC ambazo
ni Tanzania, Angola, Malawi, Lesotho, Namibia, Afrika Kusini, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo, Botswana, Zimbabwe na Zambia.
Lengo kuu la misheni hiyo ni
kukomesha matishio ya ugaidi, kuimarisha
hali ya ulinzi na usalama, kurejesha
utawala wa sheria kwenye maeneo yaliyoathirika kwenye Jimbo la Cabo Delgado na
kuisadia Msumbiji kwa kushirikiana na Mashirika yanayotoa misaada ya kibinadamu
ili kuyawezesha kutoa misaada kwenye maeneo yaliyoathirika na vitendo vya kigaidi
ikiwemo kuwasaidia watu walioyakimbia makazi yao.
Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo utaongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe. Viongozi wengine kutoka Tanzania watakaoshiriki Mkutano huo ni pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe. Meja Jenerali (Mst) Gaudence Milanzi na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Agnes Kayola.
Wajumbe wengine wa Tanzania wanaoshiriki Mkutano. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.