Waziri
wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Amerika Kusini na
Visiwa vya Karibian Mhe. Vicky Ford amewasili jijini Dodoma akiwa katika ziara ya
kikazi ya siku tatu nchini kuanzia tarehe 3 - 5 Aprili 2022.
Waziri
huyo amepokelewa katika uwanja wa ndege wa Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma Rajab.
Baada
ya kuwasili jijini Dodoma Waziri Ford alielekea Ikulu ya Chamwino ambako alikutana na kufanya mazungumzo na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznsia Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula.
Katika
ziara yake nchini Mhe. Ford pamoja na mambo mengine, anatarajiwa
kuzindua mpango mpya wa Elimu bunifu nchini ambao unafadhiliwa na
serikali ya Uingereza.
katika ziara yake nchni Waziri
Ford ataungana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf
Mkenda na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa kuzindua mpango huo mpya wa
maendeleo wa elimu bunifu nchini unaoitwa Shule Bora utakaofanyika Kibaha mkoani Pwani tarehe 04 Aprili 2022.
Mpango
wa Shule Bora utaongeza upatikanaji wa elimu kwa watoto zaidi ya
milioni nne (4) nchini, umelenga kuboresha viwango vya elimu kwa watoto
wenye ulemavu, watoto wanaotoka maeneo yenye upungufu wa rasilimali na
wasichana.
Kati ya mwaka
2015-2020 Uingereza kupitia ufadhili katika sekta ya elimu imesaidia zaidi ya watoto
milioni 15.6 duniani kote kupata elimu, ikiwa ni pamoja na wasichana
milioni 8.1.
Waziri Ford
pia atakuwa na mikutano na ziara mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kazi mbalimbali zinazofanywa nchini katika
kuimarisha uhusiano kati ya Uingereza na Tanzania kupitia nyanja za
biashara, mabadiliko ya tabianchi na kupambana na uhalifu mkubwa na
uliopangwa.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.