Na Waandishi wetu, Dodoma
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeridhia na kupitisha makadirio ya Mapato na matumizi ya Shillingi bilioni 208. 4 kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 Jijini Dodoma
Akiwasilisha bungeni hotuba yake, balozi Mulamula amelieleza Bunge kuwa ili Wizara yake iweze kutekeleza kwa ukamilifu majukumu yake kwa Mwaka wa fedha 2022/2023 ameliomba Bunge hilo Tukufu liidhinishe jumla ya shilingi bilioni 203.66 kwa ajili ya matumizi ya kawaida pamoja na shilingi bilioni 4.7 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Aidha, Balozi Mulamula ameyataja mafanikio ambayo Wizara inajivunia kwa mwaka 2021/2022 ambayo ni pamoja na kupeleka mabalozi 19 na watumishi 138 wenye fani mbalimbali balozini na kuteua mabalozi saba kuwa Wakuu wa Idara na Vitengo wizarani kwa lengo la kumarisha utendaji katika balozi za Tanzania nje na wizarani.
Rais wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Jopo la Wazee la SADC la Usuluhishi wa Migogoro kwa mwaka 2021 – 2025, na Bi. Hellen Lwegasira, aliyewahi kuwa mtumishi wa Wizara ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Timu ya Upatanishi ya SADC kwa kipindi cha miaka minne (2021-2025).
Tanzania iliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Rasilimaliwatu na Utawala ya SADC na kutokana na uenyekiti huo, Tanzania imechangia kuboresha Sera za ajira katika SADC.
Tanzania kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa Kituo cha SADC cha Kupambana na Ugaidi chenye makao makuu yake jijini Dar es Salaam pamoja na kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Amani na Usalama la AU kwa Mwaka 2022 – 2024.
Tanzania kuridhia Mkataba wa kuanzishwa kwa Eneo Huru la Biashara la Afrika na kuungana na nchi nyingine 29 kuwasilisha orodha ya bidhaa zinazokidhi vigezo vya Mkataba huo.
Wizara kufanikisha uzinduzi wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2022 - 2027 wa ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa Mataifa nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kutunikiwa Tuzo ya Super Prize Great Builder – Trophée ya Boubacar Ndiaye kutoka AfDB kwa kutambua mchango wake katika ujenzi wa miundombinu nchini
Tanzania kufungua Balozi mpya katika Umoja wa Mataifa Austria na Indonesia pamoja na Konseli Kuu mbili za Lubumbashi – DRC na Guangzhou – China na kufanya idadi ya Balozi za Tanzania nje kuwa 45 na Konseli Kuu 5
Kuongezeka kwa mchango wa Diaspora nchini kutoka Dola milioni 400 mwaka 2020 hadi kufikia Dola 569.3 mwaka 2021.
Wizara kukamilisha taratibu za ununuzi kupata wakandarasi watakaotekeleza miradi ya ujenzi na ukarabati kwenye Balozi za Tanzania za Nairobi, Kinshasa, Muscat, Moroni na Washington D.C.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 |
Sehemu ya Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukifuatilia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 |
Sehemu ya Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika picha ya pamoja na uongozi wa Wizara na wafanyakazi wa wizara |