Tuesday, May 31, 2022

WAWEKEZAJI KUTOKA NCHINI CHINA WAENDELEA NA ZIARA KUSINI MWA TANZANIA

Watendaji wa Kampuni ya Longping High Tech ya nchini China ikiongozwa Mkurugenzi wa Biashara za Nje na Fedha wa Kampuni hiyo Bw. Shangyang Wu wameendelea na ziara yao katika mikoa ya Kusini mwa Tanzania ikihusisha Ruvuma na Mbeya. Ziara hiyo ni mwendelezo wa kuonana na kufanya mazungumzo na wataalamu, watendaji na wadau wa kilimo katika mikoa hiyo ili kwa pamoja kujadili na kupanga namna bora ya kuwawezesha wakulima kuongeza ubora na uzalishaji wa maharage ya soya. 

Vilevile wawekezaji hao wa maharage ya soya, wakiwa katika mikoa hiyo kwa nyakati tofauti wamepata fursa ya kutembelea na kuona mashamba ya Taasisi na wakulima wa maharage ya soya kwa lengo la kubaini changamoto zinazowakabili wakulima, sambamba na kuangalia namna ya kutoa suluhisho la changamoto hizo.

Miongoni mwa Viongozi, taasisi na Wadau walionana na kufanya mazungumzo na wawekezaji hao ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Z. Homers, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Bw. Sajidu I. Mohamed, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) ya Uyole Mbeya Dkt. Tulole Bucheyeki, na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe. 

Katika mazungumzo na wawekezaji hao Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Homers alieleza kuwa Mkoa wa Mbeya upotayari kupokea uwekezaji wa Kampuni ya Longping High Tech huku akielezea matumaini yake kuwa uwekezaji huo utapoanza kutelezwa utaboresha hali ya maisha ya wanachi wa Mkoa huo. 

Tayari tumeshatenga zaidi ya hekari 100000 kwa ajili ya uzalishaji wa maharage ya soya, ninaamini kuwa uwekezaji wenu utaboresha zaidi hali ya maisha ya Wananchi kwa kuwaongezea kipato, pia niwahakikishie kuwa kwa bidii ya wakulima wetu na hali ya hewa rafiki kwa kilimo cha soya mtapata kiasi kikubwa cha soya kutoka kwa wananchi wetu” Alisema Mhe. Homers

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania ya Uyole (TARI), Mbeya Dkt. Tulole Bucheyeki akizungumza na wawekezaji hao alibainisha kuwa Taasisi hiyo ipo tayari kutoa ushirikiano kwa Longping High Tech katika uwekezaji wao hapa nchini. 

Watendaji wa kampuni ya Loping High Tech na ujumbe wao wanatarajia kuendelea ziara yao mkoani Katavi. 
Watendaji wa Kampuni ya Longping High Tech ya nchini China wakifuatilia maelezo kutoka kwa mtaalamu wa utafiti wa maharage ya soya wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) ya Uyole, Mbeya walipotembela moja ya shamba la Taasisi hiyo. 
Watendaji wa Kampuni ya Longping High Tech ya nchini China wakifuatilia maelezo kutoka kwa mtaalam wa Wizara ya Kilimo Bw. Revelian Ngaiza walipotembelea shamba linalotarajiwa kutumika katika uzalishaji wa soya lililopo Halmashauri ya Madaba, Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Z. Homers na Watendaji wa Kampuni ya Longping High Techwakiwa katika picha pamoja baadhi ya watendaji kutoka sekta binafsi na serikalini baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa jijini Mbeya.
Watendaji wa Kampuni ya Longping High Tech ya nchini China wakifurahia jambo katika picha ya pamoja na Watendaji kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) ya Uyole, Mbeya Watumishi kutoka Wizarani Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Kilimo na Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (“SAGCOT”) walipotembela moja ya shamba la TARI.
Watendaji wa Kampuni ya Longping High Tech ya nchini China wakifuatilia maelezo kutoka kwa mtaalamu wa utafiti wa maharage ya soya wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) ya Uyole, Mbeya walipotembela moja ya shamba la Taasisi hiyo.
Watendaji wa Kampuni ya Longping High Tech ya nchini China wakifuatilia maelezo kutoka kwa mtaalamu wa kilimo wa Kampuni ya Silverland Ndolela Limited waliotembelea shamba la kampuni hiyo lililopo Madaba, Ruvuma

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.