Mkutano ukiendelea (Picha na Reginald Philip)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SERIKALI HAIJAWATELEKEZA WATANZANIA WANAOSOMA
UKRAINE
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kukanusha vikali taarifa iliyotangazwa
na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), tarehe 30 Julai, 2014,
iliyodaikuwa Serikali ya Tanzania imetelekeza wananchi
wake wanaosoma Ukraine Mashariki, ambako kunarindima vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Taarifa
hiyo ya upande mmoja, iliyomnukuu mtu anayeitwa Shamila, aliyedai ni mmoja wa wanafunzi
Watanzania nchini Ukraine, ilisema eti wananchi hao wameachwa bila msaada wowote.
Wizara
imesikitishwa na taarifa hiyo iliyotolewa bila kufanyiwa uchunguzi wa kutosha.
Ukweli ni kwamba Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, ambao unatuwakilisha pia
Ukraine, umechukua hatua za haraka tangu mwezi Juni, 2014, kuhakikisha wanafunzi
Watanzania wote wanaondoka katika jimbo la Lugansk lililoko vitani.
Ubalozi
ulishirikiana na Rais wa wanafunzi wa Tanzania katika mji wa Lugansk, Bwana
Ahmad Juma, kufanikisha kuondoka kwa Watanzania wote 32 waliokuwepo huko kurudi
nyumbani au kuhamia mji wa Kharkov, ambao ni salama zaidi.
Serikali
kupitia Ubalozi wake Moscow iliwaombea wanafunzi hao malazi kwenye Chuo cha Kharkov
Technical University ambacho kilikubali kutoa hosteli kwa wanafunzi hao. Hata hivyo,
wengi wa wanafunzi hao waliondokea Lugansk kurudi nyumbani isipokuwa wanafunzi saba
ambao walihamia Kharkov. Mpaka tarehe 31 Julai, 2014, ni wanafunzi watatu tu waliokuwa
wamebaki mjini Kharkov. Wanafunzi 20 wamedhaminiwa na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kupitia Bodi ya Mikopo.
Orodha
ya wanafunzi iliyopo Ubalozini haijumuishi jina la Shamila anayedaiwa kuhojiwa na
BBC. Inasemeka na mtu huyo alikwishamaliza masomo yake ya shahada ya kwanza na ya
pili lakini akaamua kubakia Ukraine akifanya udalali wa kuleta wanafunzi kutoka
Tanzania kwa kushirikiana na vijana wa Nigeria.
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kuuhakikishia Umma kuwa inasimamia
kikamilifu usalama na ustawi wa Watanzania walioko Ukraine na popote ulimwenguni,
na inasikitishwa na taarifa ya uzushi, upotoshaji na uzandiki iliyomnukuu mtu anayeitwa
Shamila.
IMETOLEWA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO
WA KIMATAIFA DAR ES SALAAM
02 AGOSTI, 2014
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.