Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Chabaka F. Kilumanga (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Muungano wa visiwa vya Comoro Mhe. El-Anrif Said Hassane. |
Waziri wa mambo ya Nje wa Muungano wa Visiwa vya Comoro Mhe.
El-Anrif Said Hassane amekabidhi rasmi eneo lililotolewa na Serikali ya Comoro kwa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwaajili ya Ujenzi wa Ubalozi wa
Tanzania Mjini Moroni.
Hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika Wizara ya Mambo ya
Nje ya Comoro ambapo Mhe. Waziri El-Anrif amemkabidhi Balozi wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Chabaka F. Kilumanga funguo zamajengo matatu yaliyopo
katika eneo hilo. Tukio hilo limeshuhudiwa pia na Mhe Ahamada El-Badaoui Mohamed
Fakih, Balozi wa Comoro nchini Tanzania.
Sambamba na kukabidhiana eneo hilo, Mhe. Balozi Kilumanga na
Mhe. Waziri El-Anrif walipata fursa ya kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu
namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Comoro kwa maslahi ya pande
zote mbili.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.