Saturday, August 2, 2014

Serikali ya Comoro ya kabidhi Eneo kwa Ubalozi Tanzania nchini humo

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Commoro, Mhe. Chabaka F. Kilumanga (katikati) akionyesha funguo aliyokabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe El-Anrif Said Hassane (ikiwa) ni ishara ya kukabidhiwa eneo lililotolewa na Serikali ya Comoro kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwaajili ya Ujenzi wa Ubalozi wa Tanzania mijini Moroni
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Chabaka F. Kilumanga (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Muungano wa visiwa vya Comoro Mhe. El-Anrif Said Hassane.


Waziri wa mambo ya Nje wa Muungano wa Visiwa vya Comoro Mhe. El-Anrif Said Hassane amekabidhi rasmi eneo lililotolewa na Serikali ya Comoro kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwaajili ya Ujenzi wa Ubalozi wa Tanzania Mjini Moroni.

Hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika Wizara ya Mambo ya Nje ya Comoro ambapo Mhe. Waziri El-Anrif amemkabidhi Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Chabaka F. Kilumanga funguo zamajengo matatu yaliyopo katika eneo hilo. Tukio hilo limeshuhudiwa pia na Mhe Ahamada El-Badaoui Mohamed Fakih, Balozi wa  Comoro nchini Tanzania.

Sambamba na kukabidhiana eneo hilo, Mhe. Balozi Kilumanga na Mhe. Waziri El-Anrif walipata fursa ya kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Comoro kwa maslahi ya pande zote mbili. 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.