Mhe. Chabaka Kilumanga (wa pili kushoto), Balozi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya mazungumzo na Bw. Yogesh Manek,
Mwenyekiti wa Bodi ya Exim Bank, kwenye Makazi ya Balozi, mjini Moroni. Maudhui
ya mazungumzo hayo yalihusu azma ya Ubalozi ya kuwakutanisha wafanyabiashara wa
Tanzania na wenzao wa Comoro kwa lengo la kuwezesha kila upande kutambua
wafanyabiasha wanaotambulika na kuaminika na pia kuwahamasisha kufanya
biashara kwa kutumia taratibu rasmi. Uongozi wa Exim Bank umekubali kusaidia
kifanyanikisha azma hiyo. Mhe.
Balozi na Bw. Manek walizungumzia pia uwezekano wa Exim Bank kudhamini mradi
mkubwa wa umeme ambao unategemewa kuanzishwa kati ya Shirika la Umeme la Comoro
na Kampuni ya DACC Global ya Marekani kwa kushirikiana na Kampuni ya NSI Energy
ya Tanzania.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.