Monday, August 11, 2014

Tanzania na Jamhuri ya Korea kuimarisha ushirikiano



Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki akizungumza wakati wa mkutano kati yake na Mkurugenzi anayeshughulikia masuala ya Afrika na Mashariki ya Kati kutoka Jamhuri ya Korea Bw. KWON Hee-seog (hayupo pichani) kuhusu masuala mbalimbali katika kuimarisha ushrikiano kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea. Mkutano huo uliwahusisha pia wadau  kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za hapa nchini akiwemo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji  (EPZA), Dkt. Adelhelm Meru (mwenye miwani).
Bw. KWON Hee-seog akizungumza wakati wa mkutano wake na Balozi Kairuki (hayupo pichani)
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Kairuki na Bw. KWON Hee-seog (hawapo pichani)
Mkutano ukiendelea
Balozi Kairuki akimkabidhi zawadi Bw. KWON Hee-seog.
Balozi Kairuki na Bw. KWON Hee-seog (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Mhe. CHUNG Il na Bw. Nathaniel Kaaya, Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Asia na Australasia. 

(Picha na Reginald Philip)

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.