Na Mwandishi wetu, Dar
Mamlaka
ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeelekezwa kushirikiana na Balozi
za Tanzania katika kutangaza fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji hapa nchini.
Agizo
hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab wakati alipotembelea Maonesho ya 45 ya
Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
“…………….Balozi
zetu zina uhusiano wa karibu na TanTrade ambapo TanTrade moja kati ya majukumu
yake ni kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wetu hapa nchini wanapata taarifa
sahihi ili kusaidia kujua ni bidhaa gani za Tanzania zinaweza kuuzwa nje kwa
urahisi lakini pia kujua ni nchi husika yenye uhitaji wa bidhaa hizo,” amesema
Balozi Fatma
Balozi
Fatma ameongeza kuwa ili bidhaa za Tanzania ziendelee kuuzwa katika masoko ya
kimataifa ulimwenguni, TanTrade iendelee kushirikiana kwa karibu na Balozi za
Tanzania katika kuhakikisha kuwa inatoa taarifa sahihi za bidhaa.
“Ushirikiano
baina ya TanTrade na Balozi zetu uendelee kuimarishwa ili kuwawezesha
wafanyabiashara kupata taarifa sahihi na kwa wakati, lakini pia ushirikiano huu
utasaidia kutangaza fursa za biashara zilizopo nchini Tanzania katika Mataifa
ya Kigeni,” amesema Balozi Fatma
Balozi
Fatma pia ametoa wito kwa watanzania kutumia fursa ya maonesho ya Sabasaba
kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara kutoka nje ya Nchi walioshiriki katika
maonesho hayo ili kujua ni kwa namna gani wataweza kunufaika na fursa za kuuza
bidhaa zetu kwenye nchi za kimataifa
“Kupitia
maonesho haya watanzania watumie fursa hii kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara
kutoka nje ya Nchi walioshiriki katika maonesho haya, lakini pia kuangalia ni
namna gani watanufaika na fursa za kuuza bidhaa zetu kwenye nchi za kimataifa,”
Amesema Balozi Fatma Rajab.
|
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Fatma Rajab akisaini kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipotembelea banda la Wizara katika
Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya
Mwalimu Nyerere Dar es salaam |
|
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Fatma Rajab akipokea nakala ya Jarida la Diplomasia linalochapishwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki alipotembelea banda la Wizara katika Maonesho ya 45 ya
Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es
salaam |
|
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Fatma Rajab akimsikiliza mtumishi wa Wizara alipokuwa akimpatia maelezo juu ya
baadhi ya viongozi (Mawaziri) waliohudumu katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki tangu mwaka 1961 hadi sasa mwaka 2021 |
|
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Fatma Rajab akiongea na waandishi wa habari wakati alipokuwa katika banda la
Wizara katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika
viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam |
|
Afisa
kutoka Tume ya Utalii Zanzibar akimfafanulia jambo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab wakati
alipotembelea banda la tume hiyo katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara
yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam |
|
Afisa
kutoka Bodi ya Mapato Zanzibar akimuelezea jambo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab wakati
alipotembelea banda la Bodi hiyo katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara
yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.